135027 Wajitokeza Ajira 1596 Za TRA 2025

135027 Wajitokeza Ajira 1596 Za TRA 2025
135027 Wajitokeza Ajira 1596 Za TRA 2025
Watu 135,027 Wamejotokeza Kuomba Ajira katika nafasi 1,596 zilizotangazwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Februari 6, 2025 TRA ilitangaza nafasi za Ajira katika idara za mapato ya ndani, forodha na ushuru, usimamizi na utawala wa raslimali watu.
Nyingine ni utafiti na mipango, fedha, ukaguzi wa ndani, mambo ya ndani na idara ya viatarishi na uzingatiaji.
Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda Machi 12, 2025 wakati akielezea mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita na mwelekeo wa mamlaka hiyo.
Yusuph Mwenda amesema kuwa mwitikio wa kufanya kazi TRA umekuwa mkubwa akitolea mfano kuwa wametangaza kazi 1,596, lakini hadi wanakamilisha siku ya mwisho ya kupokea maombi walioomba walikuwa ni watu 135,027.
Aidha amesema kuwa wiki ijayo Mkurugenzi wa utawala atatoa utaratibu utakaofuatia kuhusiana na Ajira hizo.
Mwenda amewahakikishia Watanzaniaa kuweka mazingira ya haki na usawa ili kila mtu mwenye sifa apate fursa na ajira ndani ya Mamlaka ya Mapato Tanzania.
Ameongeza kuwa Mamlaka hiyo imefanikiwa kuongeza Watumishi kutoka 4,749 kabla ya Machi 2021 hadi 6,989 kufikia Machi 2025.
Amefafanua kuwa ongezeko hilo ni sawa na nyongeza ya watumishi 2,240, sawa na asilimia 47.
Walioomba Ajira hizi wamehakikishiwa kuajiriwa kabla ya Juni,2025.
TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
