74383 Watemwa Ajira za TRA 2025

74383 Watemwa Ajira za TRA 2025
74383 Watemwa Ajira za TRA 2025
Jumla ya Watanzania 74,383 kati ya 80,888 waliofanya usaili wa Kuandika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wamekosa sifa ya kuendelea Katika hatua inayofuata ya Usaili.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TRA Aprili 26, 2025, waliochaguliwa kuendelea hatua hiyo ni 6,505 ambao sasa watafanya usaili wa Mahojiano na Vitendo.
Aidha watu watakaofaulu mtihani wa mwisho watakwenda kujaza nafasi 1,596 ambazo Machi 12, 2025 TRA ilitangaza watu 135,027 kuwa ndio walioomba nafasi hizo.
Katika Nafasi zilizotangazwa ipo ya Msimamizi Msaidizi wa Kodi, ambapo Waombaji Walikuwa 5,491 na Waliofaulu Usaili wa Kuandika ni 974.
Nafasi nyingine ni ya Ofisa Forodha Daraja la Pili, waombaji walikuwa 14,614 na Waliofaulu na kuendelea na hatua inayofuata ni 862.
Katika kundi la Madereva, Waombaji walikuwa 3,480 na Waliofaulu Katika hatua inayofuata ni 553.
Nafasi zingine ni ya Ofisa Msimamizi Ushuru Daraja la II ambapo wanaohitajika ni watu 573, Ofisa Forodha Daraja la II watu 232, Msaidizi Wa Usimamizi Wa Ushuru Daraja la II, Watu 253, Msaidizi Wa Forodha Daraja la II ni watu 154 na Mhadhiri Msaidizi nafasi 15.
Wengine ni Ofisa Usimamizi data Daraja la II Nafasi 20, Ofisa Rasilimali Watu Daraja la II Nafasi 11, Ofisa Utawala Daraja la II 3, Ofisa Usafirishaji Daraja la II nafasi 5 na Ofisa Milki Daraja la II nafasi 15.
Pia wa Wahandisi Daraja la II nafasi 12, Wajiolojia Daraja la II nafasi 2, Ofisa Hesabu Daraja la II nafasi 12, Mhasibu Daraja la II nafasi 2, Ofisa Mambo Ya Ndani Daraja la II nafasi 10, Ofisa Vihatarishi Daraja la II nafasi 8 pamoja na Wachumi Daraja la II nafasi 6.
Nyingine ni Mkaguzi wa ndani Daraja la II nafasi 2, Mlinzi Daraja la II nafasi 2, Ofisa Uhusiano Daraja la II nafasi 5, Msaidizi wa Mafunzo nafasi 2, Katibu Muhtasi Daraja la II nafasi 12, Mtaalamu Wa Maabara Daraja la II nafasi 4, Ofisa Hesabu Msaidizi nafasi 10 na Msaidizi wa Usimamizi wa Rekodi Daraja la II nafasi 10.
Na Nyingine ni Mafundi Uashi na Umeme Daraja la II nafasi 10, Mwendesha Mfumo wa Ulinzi Daraja la II nafasi 9, Nahodha Daraja la II 8, Fundi Boti nafasi 8, Mkutubi Msaidizi Daraja la II nafasi 2, Nahodha Msaidizi Daraja la II nafasi 2, Mtu Wa Mapokezi Daraja la II nafasi 20, Dereva Daraja la II nafasi 105 pamoja na Msaidizi wa Ofisi Daraja la II nafasi.
Nafasi nyingine ni Watakwimu Daraja la II nafasi 4, Mwanasheria Daraja la II nafasi 6, Ofisa Ununuzi na Usambazaji Daraja la II nafasi 5, Ofisa Maabara nafasi 3, Mkutubi Daraja la II nafasi 4, Ofisa Taaluma daraja la II nafasi 2.
TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
