ADA na Gharama Za Kupata Cheti Cha Kuzaliwa

ADA na Gharama Za Kupata Cheti Cha Kuzaliwa
ADA na Gharama Za Kupata Cheti Cha Kuzaliwa
Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) ametaja Ada na Gharama Za kupata Cheti Cha Kuzaliwa.
Ada zote zimeorodheshwa hapa chini.

ADA na Gharama Za Kupata Cheti Cha Kuzaliwa
Mahitaji ya jumla kwa maombi ya cheti cha kuzaliwa:
Mwombaji lazima aambatishe baadhi ya hati mbili kati ya zifuatazo:
- Kadi ya Kliniki ya Mama
- Kadi ya Kliniki ya Mtoto
- Tangazo la kuzaliwa
- Cheti cha Ubatizo cha Mtoto (kwa wale walio batizwa wakiwa na umri mdogo)
- Cheti cha Kumaliza elimu (Shule za Msingi au Sekondari – O Level)
- Pasi ya kusafiria
- Kadi ya mpiga kura
- Cheti cha ubatizo
Pamoja na mojawapo ya haya:
- Kitambulisho cha Kitaifa cha mzazi/mlezi
- Hati ya kusafiria ya mzazi
- Utambulisho kutoka Mtendaji wa Kata
N.B: Uhitaji wa kuweka vitambulisho vya wazazi vitatumika ikiwa wazazi wapo hai.
USAJILI UNAVYOFANYIKA KWA WATOTO WACHANGA
Mwombaji (Mzazi/mlezi) atasajili tukio hili kwenye dawati la Usajili katika Kituo cha tiba kizazi kilipotokea wakati mtoto anapozaliwa au wakati wa kupata chanjo.
Pia Usajili unaweza kufanyika katika ofisi ya kata kwa vizazi vya nyumbani.
USAJILI KUPITIA ERITA (VIZAZI VILIVYOCHELEWA KUSAJILIWA)
1)Mwombaji anaweza kufanya maombi kupitia tovuti yetu www.rita.go.tz na kubonyeza menyu ya eRITA kuchagua huduma inayohitajika.
2)Mwombaji anatengeneza akaunti kwa kujisajili, kisha barua pepe itatumwa kwa mombaji ili kuthibitisha akaunti.
3)Mwombaji atahitajika kuthibitisha akaunti kwa kubonyeza kitufe kilichotumwa kwa barua pepe.
4)Ingia katika mfumo wa eRITA na kisha bonyeza kizazi nenda mbele ubonyeze cheti kipya halafu jaza taarifa zako kwa usahihi na kuchagua sehemu utakayo chukua cheti chako
5)Mwombaji atatakiwa kuwa na nakala laini (soft copies) za viambatanisho vinavyotakiwa kuwa katika mfumo wa pdf kwaajili ya kuviambatanisha pamoja na maombi yake katika mfumo nyaraka hizo ni kama zifuatavyo;
- Kadi ya Kliniki ya Mama
- Kadi ya Kliniki ya Mtoto
- Tangazo la kuzaliwa
- Cheti cha Ubatizo cha Mtoto (kwa wale walio batizwa wakiwa na umri mdogo)
- Cheti cha Kumaliza elimu (Shule za Msingi au Sekondari – O Level)
- Pasi ya kusafiria
- Kadi ya mpiga kura
Cheti cha ubatizo
Pamoja na mojawapo ya haya:
- Kitambulisho cha Kitaifa cha mzazi/mlezi
- Hati ya kusafiria ya mzazi
Utambulisho kutoka Mtendaji wa Kata
N.B: Uhitaji wa kuweka vitambulisho vya wazazi vitatumika ikiwa wazazi wapo hai
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA
(i)Ada ya utoaji wa cheti kupitia mfumo kwa matukio ya vizazi yaliyosajiliwa ndani ya muda Tshs 7000
(ii)Ada ya usajili wa kizazi kilichochelewa kuandikishwa ni Tsh 8,000 kwa tukio lililo chini ya miaka 10 na Tsh 20,000 kwa tukio zaidi ya miaka 10.
(iii)Baada ya kukamilisha kutuma maombi unashauriwa kutembelea akaunti yako kufuatailia kama yamepitishwa.
Endapo utakuta:
Neno verify ina maana maombi yamepelekwa hatua ingine kwaajili ya kuhakikiwa na Msajili
Neno return to client ina maana maombi yana kasoro na yamerudisha kwa mteja kwaajili ya kufanyia kazi malekezo ya Msajili halafu urejeshwe maombi hayo kwaajili ya kuchakatwa.
Neno approved ina maana maombi yamekidhi vigezo na yamepelekwa kwenye hatua ya kuchapishwa cheti.
Neno issued ina maana cheti chako tayari. Ingia katika akaunti yako bonyeza neno submitted ikishafunguka utabonyeza details utaona neno download ibonyeze utaona fomu yako ya maombi ichapishe na ipeleke ofisi uliochagua kuchukua cheti chako.
Angalizo, Tunapenda kusisitizia waombaji wote kufuata maelekezo hapo juu ili kuepuka usumbufu na pia tunza taarifa ulizotumia kufungua akaunti kwa ajili yakutumia mfumo na kuingia kuangalia maombi yako kama yamepitishwa.
MUHIMU: Kama umesahau nywila (Password) unaweza kufanya marekebisho kwa kuponyeza neno reset inayopatikana pembeni ya neno forget password halafu kisha rudi katika email yako uliyoitumia kufungulia akaunti utakuta ujumbe wa kureset Password bonyeza ili kuhuisha akaunti yako ambapo utathibitisha (Confirm) baada ya hapo utatengeneza nywila mpya kwaajili ya kuingia (log in) katika mfumo na kutuma maombi.
UHAKIKI WA VYETI VYA KUZALIWA
Ili uweze kuhakiki cheti cha kuzaliwa au kifo ingia kwenye mfumo kwa kutumia link ya huduma za RITA https://erita.rita.go.tz/auth au unaweza kutumia tovuti ya Wakala www.rita.go.tz na kisha utabofya katika menu ya eRITA.
Namna ya kutuma maombi aya uhakiki wa vyeti
- Bonyeza huduma ya verification
- Jaza taarifa zinazohitajika
- Ambatanisha nakala laini ya cheti chako cha kuzaliwa kwaajili ya uhakiki
- Mfumo utatengeneza ankara bill ya shilingi 6,000/= kwaajili ya kuitumia kufanya malipo
- Mwombaji atafuatilia maombi yake kwa kuingia (log in) katika akaunti yake.
- Mwombaji atapokea majibu kwenye akaunti yake. Ilia aone majibu atatakiwa kubonyeza neno submitted ikisha funguka utabonyeza details utaona hali ya ombi.
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags: ADA na Gharama Za Cheti Cha Kuzaliwa, ADA na Gharama Za Kupata Cheti Cha Kuzaliwa