Ada Za Lipa Kwa M-Pesa, Makato ya Lipa Kwa M-Pesa

Ada Za Lipa Kwa M-Pesa, Makato ya Lipa Kwa M-Pesa
Ada Za Lipa Kwa M-Pesa, Makato ya Lipa Kwa M-Pesa
LIPA kwa Simu au LIPA kwa M-pesa ni huduma ya kisasa na jumuishi ya mfumo wa malipo utakao wezesha Makampuni, Mawakala wa jumla na rejareja na Wafanyabiashara wengine kulipia bidhaa zao kwa kutumia M-PESA.
Huduma hii ya LIPA kwa Simu imekuja ili kuboresha mazingira ya Wafanyabiashara na Makampuni kwa kupanua mbinu za malipo kutoka kwa wafanyabiashara na Makampuni na Wauzaji wa aina mbalimbali.
Mawakala wa jumla na rejareja wataweza kununua na kulipia bidhaaa zao kwa kutumia huduma hii ya LIPA KWA M-PESA au LIPA KWA SIMU, Njia hii ni ya haraka, salama na inampa mteja wepesi zaidi wa kufanya biashara.
Mfanyabiashara atakuwa na Lipa namba na QR code ambazo zitaruhusu wateja kulipia bidhaa kwa kuingiza Lipa namba au kuskani picha ya QR.
Lipa Kwa Simu imewawezesha wateja wa mitandao na benki zote kufikia malipo kwa urahisi, usalama ukilinganisha na fedha taslimu ambazo ni za gharama na hatari ndiyo maana tunasema M-Pesa nyumbani kwa malipo ya kidijitali.
Kwa kutumia msimbo wa QR ulioboreshwa ambao hurahisisha matumizi ya malipo zaidi kwa kuondoa hitaji la kuandika hadi nambari katika sehemu za kugusa rejareja.
Lipa Kwa Simu inaweza kutumika katika maduka mbalimbali katika mtaa wako k.m. migahawa, maduka ya rejareja, vituo vya mafuta, saluni, baa, maduka makubwa, maduka ya vifaa vya ujenzi, maduka ya dawa na maduka mengine yoyote.
Kwa msaada piga 100/101, WhatsApp 0754100100 au tuma barua pepe kwa support@vodacom.co.tz
MAKATO ya Lipa Kwa M-pesa, Ada za Lipa Kwa Simu
Unapofanya malipo kwa wafanyabiashara waliosajiliwa katika huduma ya LIPA KWA M-PESA utatozwa ada ndogo ya 0.5% ya kiasi unacholipa kwa malipo yote ya hadi Tsh 1,500,000/=.
Kwa msaada zaidi wasiliana na huduma kwa wateja kwa kupiga namba 100 bure.
Amount From (Tsh) | Amount To (Tsh) | Fees (Tsh) |
---|---|---|
100 | 999 | 20 |
1,000 | 1,999 | 50 |
2,000 | 2,999 | 70 |
3,000 | 3,999 | 100 |
4,000 | 4,999 | 200 |
5,000 | 6,999 | 300 |
7,000 | 9,999 | 500 |
10,000 | 14,999 | 700 |
15,000 | 19,999 | 850 |
20,000 | 29,999 | 920 |
30,000 | 39,999 | 1,000 |
40,000 | 49,999 | 1,200 |
50,000 | 99,999 | 1,700 |
100,000 | 199,999 | 2,000 |
200,000 | 299,999 | 2,600 |
300,000 | 399,999 | 3,000 |
400,000 | 499,999 | 3,300 |
500,000 | 599,999 | 4,500 |
600,000 | 699,999 | 5,500 |
700,000 | 799,999 | 5,700 |
800,000 | 899,999 | 6,000 |
900,000 | 1,000,000 | 6,000 |
1,000,001 | 3,000,000 | 6,000 |
3,000,001 | 10,000,000 | 6,000 |
Ikiwa unahitaji Lipa number kwaajili ya Biashara yako tutumie ujumbe WhatsApp namba 0756658100 tukutengenezee na huduma hii ni Bure.
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags: Ada Za Lipa Kwa M-Pesa, Ada za Lipa Kwa Simu, MAKATO ya Lipa Kwa M-pesa
Asanteni kwa huduma hii safi na salama kwa wafanya biashara