AJIRA Mpya 33212 UTUMISHI, Ajira 10000 Za Walimu

AJIRA Mpya 33212 UTUMISHI, Ajira 10000 Za Walimu
AJIRA Mpya 33212 UTUMISHI, Ajira 10000 Za Walimu
Rais Samia Suluhu Hassan Ametoa Kibali Cha Ajira kwa nafasi 33,212 za mwaka wa fedha unaoisha 2024/25 huku Kada ya Walimu ikipangiwa Kupata Nafasi 10,000 ambazo hazitafanyiwa usaili watachukuliwa kwenye Kanzidata.
Akihitimisha jioni hoja ya makadirio ya mapato na matumizi ya Mwaka 2025/26 bungeni, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, amesema “Katika kada ya walimu tutakwenda kwenye kanzidata tuendelee kupakua waliosalia ili kuhakikisha tunawamaliza, sio rahisi kuwamaliza maana waliofaulu wanaosubiri kupangiwa bado ni wengi.”
“Wamefanyiwa usaili na wapo tayari kufanya kazi na ndio maana walipokuja vijana wa NETO nikasema acha tuzungumze kusema kweli wana haki ya kusikilizwa na vijana wale walikuwa na mambo makubwa sana na mimi niliwaelewa, niseme kama tumejenga miundombinu ya elimu kwanini tusiongeze idadi ya walimu ili kukidhi mahitaji yanayotakiwa.”
“Nataka niwasemee vijana wa NETO maana huko wanasemwa sana na wenzao, wanasema tunasema uchumi wetu umekuwa sasa ni uchumi wa kati lakini tukisoma ripoti ya CAG tunaona kuna hela imepotea tunafikiri hii yote ingeangaliwa tungepata ajira sisi ya kuziba hili gap kwenda kufundisha wetu ambao ni watoto wanaohitaji elimu, sasa ukisikia hoja kama hiyo mzazi unasema mtoto huyu ni mkorofi? Mtoto anaomba kazi utasemaje mkorofi, sio mkorofi na kazi ya serikali ni kuendelea kutafuta fursa kuajiri kwa mahitaji ya serikali.”

“Jitihada za serikali katika kipindi hiki cha Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ajira mpya zilizokuwa zimejazwa ni takriban ajira 149,000, lakini ajira mbadala ambazo Rais Samia Suluhu Hassan alitoa kibali ni 39,963. Hivi juzi, Mheshimiwa Rais ametoa kibali cha ajira nyingine ambazo zinatakiwa zijazwe kabla ya kuisha kwa mwaka huu wa fedha, ajira 33,212.” – Deus Sangu, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Naomba ajira jamani ya uuguzi
Nimekaa takriban miaka kumi nyumbani naomba kazi popote pale ndani na nje ya nchi Kama Kuna fursa please remember me,,,
Naomba kazi
na wasio kuwepo kwenye kwenye kazidata tunaomba wafikiliwe hasa elimu ya awali maana ajira zilizopita walimu wa awali lllA walikuwa wachache tunaomba tutazamwe na sisi
polee sana kaka
Naitwa YOHANA SERMAN .Kwangu mimi naona iko powa sana sana. Sasa watanzania wenzangu hii ni furusa tutake nini tena kutoka kwa rais wetu. Kama ajila zipo nawatu wakutumikia hizo ajila tunao. Basi sasa tumuunge mkono rais wetu mama yetu samia suruhu hasani. Kwakutupa furusa nzuri kama hizi. Mimi binafisi itoshe kusema rais wetu asante sana kwahaya yote, mema unayo tutendea mungu akubaliki atubaliki sanasana. Wa TANZANIA wote sema ame. kwama wasiliano. kunipata. piga +255625283952, +255780426197. Asanteni sana wote.
Ko kaupiga mwingi kwa mtazamo wako eti!
naomba ajira jamani nimekaa nyumbani takribani miaka mi4 sina kazi yoyote mimi nina elimu ya form4
kazi
Naomba ajira jamn mimi mwalimu mahiri
Naomba kazi jamani nimesomea public administration..nimemalixa 2014,
Naomba ajira jamani wazazi wetu wametusomesha kwa shida jamn wanataka nao wale matunda yetu
Tunakushuuru mama yetu na MUNGU ukulinde uwe na SIA njema kikubwa mtukumbuke tu maana NIA na UWEZO wa kufanya KAZI ya UALIMU kwa kuelimisha watoto wetu Tunayo AMINA sana mafanikio mema MIAKA 5 katika uongozi wkoInayofuata pia siku njema ya MEI MOSI 2025 kwa watenda kazi na watumishi wote Tanzania bara na Tanzania visiwani
Kwa sifa hizo! Ajira ni kakakuona
Nina miaka mi4 baada ya kuhitimu, PA 👏 Siku nikiipata Nitalitukuza zaidiii Taifa letu, kikubwa tuangalie namna ya kuajiri jamn hizi interview siyo fair
Tupeni ajira hizo tulitumikie Taifa letu jamani. Mimi nimesomea LOCAL GOVERNMENT ADMINISTRATION katika chuo pendwa cha LGTI-HOMBOLO DODOMA
Mama sisi tunakupenda sana unaupiga mwingií miaka minne sasa sina ajira nimesoma wameuza mpk viwanja wakijua nitawakomboa lakini hatimaé nipo na vyeti vyanguu ni interview tuuh unarudii huitwíii kazinii mama mtukumbuke na sisi ma afsa mifugo jamn tupo weng pia
Ila Kwa unavofanya mitano tena , najua kwenye mitano tena sitokosa ajira
Mama tukumbuke na sisi maafsa mifugo jaman
Nipeni kazj sina kazi elimu kidato cha4
natoa pongezi kwa serikali yetu sikifu.mama sisi tunakushukru sana sana. mungu akujalie afya njema
Habari? Mimi ni mwalimu mhitimu wa mwaka 2015. Nilipoteza cheti na siku ya usaili sikuruhusiwa kuingia kwenye usaili ingawaje nilikuwa na nakala ya cheti hicho. Nilikuwa nimetuma maombi chuoni kuhusu kupatiwa cheti kingine. Wiki moja baada ya tarehe ya usaili kupita, niliambiwa kuwa cheti kipo tayari na sasa tayari ninazo documents zote. Naomba msaada kuwa nifanyeje ili niweze kuingia kwenye mfumo wa ajira kwani nazeeka bila kufanyia kati taaluma yangu ya ualimu.
Nenda Dodoma kitaeleweka huko
Tunakushukru sana Rais wetu mteule Kwa kutujali Watanzania Kwa kutupa fursa mbalimbali za kazi,Mungu akubariki Amina
Naomba kazi .nimesoma afya ya jamii ni mwaka wa sana sasa Bado sijafanikiwa
Ukiachana na za walimu zingine ni gani???
Simon paschal MAMA tunakushukuru sana kwa kuendelea kutoa ajira na hongera kwa kazi nzuri pamoja na wasaidizi wako ukweli kazi inafanyika na inaonekana japo hata kama utatenda mema na kutoa nafsi yako bado kuna Wale ambao wanaona hufanyi kazi nao hao ni mawazo yao na fikra zao (maana MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA).Basi kwa hayo machache napenda kuomba kukumbukwa na mie maana nina miaka saba najitolea kufundisha kwa moyo wote lakini ajira zikitoka sikumbukwi,nawaomba nami wanikumbuke.ujumbe uchaguzi na kushiriki kupiga kura ni haki na chachu ya maendeleo kwa TAIFA twende oktoba tukamthibitishe mama kwa kishindo.