Ali kamwe Aachiwa na Polisi Kwa Sharti

Filed in Michezo by on April 3, 2025 0 Comments
     
Ali kamwe Aachiwa na Polisi Kwa Sharti

Ali kamwe Aachiwa na Polisi Kwa Sharti

Ali kamwe Aachiwa na Polisi Kwa Sharti

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Afisa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga, Ally Kamwe ameachiwa huru kwa dhamana na Jeshi la Polisi Mkoani Tabora baada ya kukamatwa saa saba usiku wa kuamkia leo kwa madai ya kutoa kauli chafu kwa viongozi wa Serikali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao leo mchana Aprili 3, 2025 amethibitisha jeshi hilo kumwachia Kamwe huku akieleza kuwa anatakiwa kuripoti kituoni hapo Aprili 21, 2025.

Kamwe alishikiliwa ikiwa ni siku mbili zipite tangu arushe dongo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha katika hamasa kuelekea mchezo wao dhidi ya Tabora United uliomalizika jana Aprili 2, 2025 kwa Yanga kushinda bao 3-0.

Katika video inayosambaa mitandaoni inamuonyesha Kamwe akiwa mkoani Tabora akifanya hamasa ya mchezo huo huku akisema: “Kuna watu wanatafuta kiki..mkuu wa mkoa nani huyu, Chacha eenh? Atachacha kweli baada ya mechi,”

Chanzo cha Kamwe kusema hivyo ni kutokana na mkuu wa mkoa kuahidi Tabora United endapo itamfunga Yanga itapewa bonansi ya Sh60 milioni huku pia akishutumu watu wa Yanga kuwatumia meseji za rushwa wachezaji wa Tabora.

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *