Azam TV yapata hasara kuahirishwa mechi ya Yanga vs Simba

Filed in Michezo by on March 8, 2025 0 Comments
     
Azam TV yapata hasara kuahirishwa mechi ya Yanga vs Simba

Azam TV yapata hasara kuahirishwa mechi ya Yanga vs Simba

Azam TV yapata hasara kuahirishwa mechi ya Yanga vs Simba

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Azam Media Limited (AML) inasikitishwa na tangazo la kuahirishwa kwa mechi iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kati ya Yanga SC na Simba SC ambayo ilipaswa kufanyika leo Jumamosi Machi 8, 2025 kuanzia saa 1:15 usiku katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Tukio hilo limeleta athari kubwa kwa mashabiki wa soka, wateja, na wadau wa mpira wa miguu kwa ujumla
mkuu wa maendeleo.

Hata hivyo, Azam kama mdau mkuu wa maendeleo ya soka nchini, wanasema kuwa wamejitahidi kuhakikisha mashabiki wanapata burudani bora kupitia matangazo ya moja kwa moja, lakini hali hii iliyojitokeza ipo nje ya uwezo wao.

Tayari timu ya matangazo yakiwemo magari ya kurushia matangazo, kamera, mitambo mingine ya kurushia matangazo na timu nzima ya uzalishaji ilikuwa ipo Uwanja wa Benjamin Mkapa kwaajili ya mechi hiyo.

Azam inasema kuwa Kuahirishwa kwa mchezo huo kumesababisha hasara kubwa kutokana na gharama za maandalizi, matangazo ya kuhamasisha mechi kwa vyombo mbalimbali vya habari, usumbufu kwa kampuni zinazotangaza bidhaa na huduma na wateja wanaolipia kuangalia mpira kwenye visimbuzi vya Azam TV.

Azam TV imeongeza kuwa inaelewa matarajio makubwa ya mashabiki na wateja, na wtaendelea kuwa mstari wa mbele katika kurusha matangazo yenye ubora wa hali ya juu kwa mechi zote za Ligi Kuu ya NBC na mashindano mengine.

Azam TV imemaliza Kwa kuwaomba mashabiki, wateja na wadau wengine wanaowaunga mkono kwa kutangaza bidhaa na huduma zao kupitia matangazo ya mpira waendelee kuwa na imani nao huku wakifuatilia kwa ukaribu kwa mamlaka za soka kujua hasa nini kimetokea na hatua gani zitachukuliwa.

Pia Azam TV imesema kuwa inaangalia namna ambavyo mikataba inavyoweza kuwalinda na kadhia kama hii siku za usoni.

Azam TV yapata hasara kuahirishwa mechi ya Yanga vs Simba

Azam TV yapata hasara kuahirishwa mechi ya Yanga vs Simba

TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!