CAS Yathibitisha Kupokea Barua ya Rufaa ya Yanga

Filed in Michezo by on April 1, 2025 0 Comments
     
CAS Yathibitisha Kupokea Barua ya Rufaa ya Yanga

CAS Yathibitisha Kupokea Barua ya Rufaa ya Yanga

CAS Yathibitisha Kupokea Barua ya Rufaa ya Yanga

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) imepokea rasmi rufaa iliyowasilishwa na Klabu ya Young Africans SC dhidi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na Klabu ya Simba kufuatia uamuzi uliotolewa TPLB wa kuahirishwa Derby ya Kariakoo iliyotakiwa kupigwa Machi, 8 2025.

Kwa mujibu wa barua ya CAS walalamikiwa, TFF, TPLB na Simba wamepewa siku 10 kuanzia tarehe ya kupokea taarifa hiyo ili kuandaa na kuwasilisha utetezi wao.

Kesi hiyo itasikilizwa kwa haraka chini ya kumbukumbu namba CAS 2025/A/11298 huku pande zote zikitarajiwa kuwasilisha vielelezo na hoja zao ndani ya muda uliopangwa.

Katika barua hiyo, CAS inawajulisha wadaawa kuhusu hatua za kisheria zinazofuata, ikiwa ni pamoja na:

Uwasilishaji wa Hati za Rufaa – CAS imeambatanisha nakala ya rufaa na nyaraka muhimu kwa wadaawa ili waweze kujibu rasmi.

Uwasilishaji wa Nyaraka za Ushahidi – Young Africans inapaswa kuwasilisha ushahidi na maelezo ya kina kuhusu rufaa yao ndani ya siku 10 baada ya muda wa rufaa kumalizika.

Utawala wa Kesi – CAS imeomba wadaawa kutoa maelezo ya mawakili wao kwaajili ya mawasiliano rahisi. Pia, CAS inawataka wajibu rufaa ndani ya siku 20 baada ya kupokea nyaraka za rufaa.

Njia ya Mawasiliano – Wadaawa wanapewa fursa ya kutumia jukwaa la e-Filing la CAS kwaajili ya kuwasilisha nyaraka badala ya kutuma kwa njia ya barua.

Gharama za Kesi – Young Africans tayari imelipa ada ya CHF 1,000 kwa CAS, lakini wadaawa watatakiwa kulipia gharama za ziada za usuluhishi kama itakavyotakiwa.

Uteuzi wa Mwamuzi – Young Africans imependekeza kesi ishughulikiwe na mwamuzi mmoja badala ya jopo la waamuzi. Wadaawa wanatakiwa kujibu ikiwa wanakubali au wanapendelea jopo la waamuzi.

Lugha ya Kesi – Young Africans imeomba mchakato wa rufaa ufanyike kwa Kiingereza. Wadaawa wanapewa siku 3 kupinga hili kama wana sababu za msingi.

Maombi ya Hatua za Dharura – Young Africans imeomba hatua za muda wakati kesi ikiendelea, na wadaawa wanatakiwa kujibu ndani ya siku 10.

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *