CHADEMA Kutoshiriki Uchaguzi Mkuu 2025

CHADEMA Kutoshiriki Uchaguzi Mkuu 2025
CHADEMA Kutoshiriki Uchaguzi Mkuu 2025
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima amesema kuwa Chadema ambayo haikusaini kanuni za maadili ya uchaguzi, haitashiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu na chaguzi zote ndogo zitakazofuata kwa muda wa miaka mitano.
Kanuni hizo zimesainiwa leo Aprili 12, 2025 na vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, Serikali na (INEC) jijini Dodoma.
“Chama cha Chadema ambacho hakikusaini kanuni za maadili ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2025, hakitashiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu na chaguzi zote ndogo zitakazofuata kwa muda wa miaka mitano.” amesema Kailima.
Awali, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika alisema haendi na hajatuma mwakilishi kwenda kusaini kanuni hizo.
Mnyika kupitia mtandao wa kijamii wa X na amesema haendi na hajatuma mwakilishi kwenda Dodoma kusaini kanuni za maadili ya uchaguzi.
Alipoulizwa ni kwa nini hajateua mwakilishi Mnyika amesema: “Ni vyema mkaandika kwamba sijakwenda wala sijateua mtu. Habari kubwa sasa hivi ni katibu mkuu, sitakwenda kusaini wala sijateua mtu.”
Vyama ambavyo vimehudhuria hafla hiyo ni ADC, Demokrasia Makini, DP, NRA, NLD, SAU,UDPD, ADA- TADEA, AAFP, CCM, CUF, ACT-Wazalendo, CHAUMMA, UMD, TLP, NCCR-Mageuzi, CCK, UDP.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
