Elimu ya Msingi mwisho darasa la 6 Kuanzia 2027

Filed in Habari by on March 4, 2025 0 Comments
     
Elimu ya Msingi mwisho darasa la 6 Kuanzia 2027

Elimu ya Msingi mwisho darasa la 6 Kuanzia 2027

Elimu ya Msingi mwisho darasa la 6 Kuanzia 2027

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema kuwa elimu ya msingi itaishia darasa la sita kuanzia mwaka 2027, akimaanisha wanafunzi wa darasa la nne mwaka huu ndio wataanza kumaliza elimu yao ya msingi wakiwa darasa la sita mwaka 2027.

Waziri Mkenda amekumbusha hayo katika Mkutano wa Umoja wa Maafisa Elimu wa Mkoa na Halmashauri uliofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, Machi 4, 2025.

Aidha, Waziri Mkenda amefafanua kuwa elimu ya lazima nchini itakuwa ya miaka kumi, ambapo elimu ya msingi itakuwa ya miaka sita na sekondari itakuwa ya miaka minne.

Waziri Mkenda pia amebainisha kuwa elimu ya sekondari itakuwa na muktadha wa aina mbili: mkondo wa elimu jumla, ambayo itahusisha masomo ya darasani, na mkondo wa elimu ya amali, ikijumuisha ufundi na ujuzi katika sekta mbalimbali kama vile muziki, uvuvi, kilimo, na michezo.

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *