Feisal Salum Abdallah atajwa Simba SC

Feisal Salum Abdallah atajwa Simba SC
Feisal Salum Abdallah atajwa Simba SC
Klabu ya Simba imetajwa kuwa katika mchakato wa kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa Azam Fc, Feisal Salum Abdallah.
Inaelezwa kuwa Rais wa heshima wa Simba Bilionea Mohammed Dewji ‘Mo’ alifanya mazungumzo na Wawakilishi wa Feisal ambapo kimsingi Feisal amepewa ofa nono ya Mshahara na dau la Usajili.
Hatua iliyobaki ni Simba kufanya mazungumzo na Klabu ya Azam Fc ambayo bado inamkataba wa mwaka mmoja na Feisal Salum aliyetua hapo misimu miwili iliyopita akitokea Yanga.
Simba ina mpango wa kufanya vizuri msimu ujao wa 2025/2026 kwenye Michuano ya CAF kama walivyofanya msimu huu katika michuano ya kombe la Shirikisho Simba ikitinga fainali ambapo itacheza na RS Berkane
Feisal Salum amekuwa mchezaji wa muhimu pale Azam Fc, ambapo katika misimu miwili amefunga mabao 23 na kutoa pasi 21 za mabao.
Feisal Salum anatua Simba kuongeza nguvu kwani Jean Charles Ahoua ndiye tegemeo katika la kiungo cha Ushambuliaji Cha Simba Kwa Sasa.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
