Halmashauri ya Mji Kibaha sasa ni Manispaa

Filed in Michezo by on January 27, 2025 0 Comments
     
Halmashauri ya Mji Kibaha sasa ni Manispaa

Halmashauri ya Mji Kibaha sasa ni Manispaa

Halmashauri ya Mji Kibaha sasa ni Manispaa

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa, amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameupandisha hadhi Mji wa Kibaha, Mkoa wa Pwani, kutoka Halmashauri kuwa Manispaa.

Mchengerwa ameeleza kuwa taratibu za mwisho zinafanywa, na kutatangazwa rasmi kuwa Manispaa hivi karibuni.

Ameyaeleza hayo katika mkutano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Pwani uliofanyika Leo tarehe 27 January 2025 Mailmoja, Kibaha, mkutano ulioandaliwa kupongeza na kuunga mkono azimio la mkutano Mkuu maalum wa CCM uliofanyika Dodoma, kumchagua Mwenyekiti CCM Taifa Dkt Samia Suluhu Hassan kugombea kiti cha Urais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika uchaguzi Mkuu wa October 2025.

Mchengerwa alisema kuwa tangu Rais Samia aingie madarakani, tayari ameunganisha vitongoji kuwa vijiji na vijiji kuwa miji kulingana na vigezo na utaratibu ulio wazi.

“Kwa namna mji wa Kibaha ulivyokuwa, hakuna sababu mji huu usiwe Manispaa. Rais Samia kwa kushirikiana na viongozi wa mkoa, wilaya, na jimbo, ameleta maendeleo makubwa Kibaha na Mkoani Pwani, na hayo ni manufaa ya vizazi vijavyo,” alisema Mchengerwa.

Alifafanua zaidi kuwa hakuna anayekataa kwa macho kwamba Rais Samia amefanya kazi inayoonekana na ameacha alama katika sekta zote, huku wananchi wakiwa mashahidi wa maendeleo hayo.

Kwa mujibu wa Mchengerwa, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Pwani (MNEC), mkoa huo ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa kura, na watahakikisha hakuna kura inayopotea wakati wa uchaguzi.

TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!