HESLB Wanafunzi 873 wa Stashahada Wapata Mikopo 2025

HESLB Wanafunzi 873 wa Stashahada Wapata Mikopo 2025
HESLB Wanafunzi 873 wa Stashahada Wapata Mikopo 2025
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu HESLB inawatangazia wanafunzi wote walioomba mikopo kwaajili ya dirisha la mwezi Machi, kwamba jumla ya waombaji 873 wamepangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 1,944,922,500.00.
Katika awamu hii, mikopo imepangwa kama ifuatavyo:
- Chakula na Malazi (MA) yenye thamani ya TZS 1,519,788,750.00.
- Ada ya Mafunzo (TU) yenye thamani ya TZS 408,433,750.00 na
Vitabu na viandikwa (BS) yenye thamani ya TZS 16,700,000.00.
Kwa taarifa hii, wanafunzi walioomba mikopo wanashauriwa kuangalia taarifa zao kupitia akaunti walizoombea mikopo (SIPA).
Wanafunzi husika pia watatakiwa kujisajili katika mfumo wa malipo wa kidigitali (DiDis) kupitia Maafisa Mikopo wa vyuo vyao.
Itakumbukwa kuwa Dirisha la mwezi Machi lilifunguliwa tarehe 15 Januari 2025 hadi 15 Februari 2025.
Hadi kufikia tarehe 02 Mei,2025, jumla ya wanafunzi 8,438 wa stashahada wamenufaika na mikopo yenye thamani ya TZS 22,072,267,601.00 kwa mwaka 2024/2025.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
