IFAHAMU historia ya Papa Francis

IFAHAMU historia ya Papa Francis
IFAHAMU historia ya Papa Francis
Papa Fransisko, jina lake halisi Jorge Mario Bergoglio alikuwa askofu wa Roma, na hivyo pia Papa wa Kanisa Katoliki Duniani kote, tangu tarehe 13 Machi 2013 hadi tarehe 20 Aprili 2025.
Alimrithi Benedict XVI, ambaye alifariki mwaka 2022 akiwa Papa wa kwanza kustaafu kwa hiari baada ya takribani miaka 600.
Papa Francis alikuwa Kardinali wa Argentina, na alikuwa na umri wa miaka sabini alipokuwa Papa mwaka 2013 na kuwa Papa wa 266 katika orodha ya Mapapa.
Papa Francis alizaliwa tarehe 17 Desemba 1936 huko Buenos Aires, mji Mkuu wa Argentina, hivyo ni papa wa kwanza kutokea bara la Amerika.
Yeye ni mtoto mkubwa kati ya watoto watano, Wazazi wake walikimbia nchi yao ya asili ya Italia ili kuepuka maovu ya ufashisti.
Alipenda mchezo wa tango (ngoma ya asili ya Argentina) na akawa shabiki wa klabu yake ya soka ya mtaani ya, San Lorenzo.
Alipona baada ya kuugua nimonia, na kufanyiwa upasuaji wa kuondoa sehemu ya pafu lake, na hilo lilimuacha katika hatari ya kuambukizwa katika maisha yake yote.

Papa Francis akiwa kijana
Papa Francis akiwa kijana alifanya kazi kama mlinzi wa klabu ya usiku na kufanya kazi ya ufagiaji, kabla ya kuhitimu chuo kama mwanakemia.
Alifanya kazi katika kiwanda cha ndani na Esther Ballestrino, mwanaharakati aliyefanya kampeni dhidi ya udikteta wa kijeshi wa Argentina. Mwanamke huyo alitekwa, akapotea na hakupatikana tena.
Baada ya masomo ya kemia na kipindi kifupi cha kazi, tarehe 11 Machi 1958 aliitikia wito wa kitawa na wa kipadri, akaweka nadhiri za muda tarehe 12 Machi 1960, akapata upadrisho tarehe 13 Desemba 1969.
Akawa Mjesuti, akasoma falsafa na kufundisha fasihi na saikolojia, alitawazwa muongo mmoja baadaye, na kuwa Mkuu wa mkoa wa kanisa hilo nchini Argentina 1973.
Kati ya miaka 1973 na 1979 alikuwa Mkuu wa shirika nchini Argentina, Mwaka 1992 alichaguliwa kuwa askofu msaidizi wa Buenos Aires akapewa daraja hiyo tarehe 27 Juni mwaka huo, halafu akawa askofu mkuu wa Buenos Aires tarehe 28 Februari 1998, pia askofu wa Wakatoliki wa Mashariki wa Argentina wasio na askofu wa kwao tarehe 6 Novemba 1998, akateuliwa kuwa kardinali tarehe 21 Februari 2001.
Kati ya miaka 2005 na 2011 alikuwa rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki la Argentina, alichaguliwa Papa tarehe 13 Machi 2013, wiki mbili baada ya mtangulizi wake kung’atuka.
Hata kabla ya kuchaguliwa alijulikana kwa unyenyekevu na ufukara wake, pamoja na juhudi za kutetea haki za wanyonge, imani sahihi na maadili ya Kanisa.
Tabia hizo alizileta katika ngazi ya juu ya Kanisa Katoliki, akijivutia mioyo ya watu wengi.
Tarehe 13 Aprili 2013 alichagua Jopo la Makardinali 8 kutoka mabara yote limsaidie kuongoza Kanisa na kurekebisha idara na ofisi zake huko Vatcan.
Tarehe 29 Juni 2013, Papa Fransisko alitoa waraka wake wa kwanza, “Lumen Fidei”, kuhusu imani; huo ulifuatwa tarehe 24 Novemba 2013 na “Evangelii Gaudium” kuhusu uinjilishaji.
Tarehe 18 Juni 2015, alitoa barua ensiklika kwa watu wote “Laudato si'” kuhusu mazingira, mabadiliko ya hali ya hewa na maendeleo ya kufaa. Barua hiyo ilipokewa vizuri na wengi.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
