JINSI ya Kuedit Taarifa Zako Kwenye Mfumo wa Ajira Portal

Filed in Makala by on April 8, 2025 0 Comments
     
JINSI ya Kuedit Taarifa Zako Kwenye Mfumo wa Ajira Portal

JINSI ya Kuedit Taarifa Zako Kwenye Mfumo wa Ajira Portal

JINSI ya Kuedit Taarifa Zako Kwenye Mfumo wa Ajira Portal

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

JINSI ya kubadili taarifa zako Ajira Portal, Jifunze hapa namna ya kubadili taarifa ajira Kupitia Ajira Portal, Jinsi ya kuedit document kwenye mfumo wa Ajira Portal, na Jinsi ya kurekebisha nakala zako kwenye mfumo wa Ajira Portal UTUMISHI.

Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ilianzishwa kwa mujibu wa kifungu 29 (1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298 iliyorejewa 2019, ambayo inaelekeza kuwepo kwa chombo maalumu cha kushughulikia mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma.

Jukumu la msingi la Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni kuwezesha mchakato wa ajira katika Utumishi wa Umma kwa kushirikiana na Idara na Taasisi mbalimbali za Umma.

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma hutangaza nafasi za kazi mbalimbali na watanzania wenye sifa wanatakiwa kuomba nafasi hizo kupitia mfumo wa Ajira Portal.

Katika mfumo huo muombaji anatakiwa kupakia nakala za vyeti vyake ambazo zimehakikiwa na kugongwa mhuri na Mwanasheria au Wakili kuonesha kuwa ni nakala kutoka katika vyeti halisi.

Pia Muomba kazi anatakiwa kupakia vyeti vyake kwenye mfumo kulingana na kiwango chake cha Elimu ili kumuwezesha kuomba pindi nafasi zinapo tangazwa.

Ikitokea umeudanganya mfumo au umeweka cheti cha taaluma kisicho cha kwako, au unataka kuomba nafasi ya juu au ya chini kulinganisha na cheti cha taaluma ulichonacho, hutoweza kuomba nafasi uliyoomba kwani mfumo unatambua cheti chako cha elimu ambacho umeweka kwenye mfumo.

Ikitokea umekosea kupakia cheti chako, Mfumo hautokuruhusu kufuta cheti chako bali utalazimika kwenda sehemu uliyokosea na kuhariri (edit) cheti chako kisha kupakia tena (upload) kilicho sahihi.

Hata hivyo; Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inatambua changamoto wanazokutana nazo waombaji kazi hivo imeweka simu ya huduma kwa wateja namba 0262160350 inayopatikana kuanzia saa 2.00 Asubuhi mpaka saa 12.00 Jioni kwa siku za kazi na Maafisa wapo tayari kwaajili ya kutoa huduma pia unaweza kutuma barua kupitia ict@ajira.go.tz.

Pia kwa Msaada zaidi unaweza kufika katika Ofisi zetu zilizopo Dodoma katika majengo ya Dr. Asha Rose Migiro, Dar es Salaam – Magogoni, na Zanzibar – Mazizini (Jengo la sheria, Ghorofa ya tatu) kwa ajili ya msaada zaidi.

Aidha, tunawasihi waomba kazi kujaza taarifa na kupakia nakala za vyeti vyao kwenye mfumo wa Ajira portal wao wenyewe na si kufanyiwa na mtu mwingine ili kuepuka makosa yanayoweza kuepukika, na pia mnatakiwa kuzingatia taratibu na masharti yaliyoekwa kwani watanzania wengi wameweza kuomba kazi na kufanikiwa.

Epuka Matapeli, soma maelekezo kabla ya kupakia vyeti vyako na kuomba nafasi ya kazi uliyo kusudia.

Lynn Chawala
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *