JINSI ya Kufanya Marekebisho ya Majina ya Cheti NECTA Online

Filed in Elimu by on April 11, 2025 0 Comments
     
JINSI ya Kufanya Marekebisho ya Majina ya Cheti NECTA Online

JINSI ya Kufanya Marekebisho ya Majina ya Cheti NECTA Online

JINSI ya Kufanya Marekebisho ya Majina ya Cheti NECTA Online, NECTA eServices.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Baraza la Mitihani la Tanzania hushughulikia maombi ya marekebisho ya majina ya watahiniwa yaliyokosewa kuandikwa katika mitihani ya Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu.

Ufuatao ni utaratibu unaotumika katika kuwasilisha maombi na kufanya marekebisho.

Masharti Ya Marekebisho Ya Majina

  • Maombi ya marekebisho yawasilishwe katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja baada ya matokeo ya mtihani kutolewa.
  • Marekebisho ya jina ni lazima yawe na engo la kufanya jina linalohitajika lifanane na jina lililotumika katika mtihani wa sifa (awali).
  • Marekebisho yanayokusudia kuongeza jina jipya au kuondoa/ kubadilisha jina (Mfano: Magina kuwa Madoba) hayaruhusiwi.
  • Marekebisho yanayolenga kuboresha herufi zisizoathiri Matamshi ya jina linapotamkwa yanaweza kuombwa kufanyika.
  • Msingi pekee wa marekebisho ya jina ni mtihani wa sifa (awali) na sio jina lililopo katika viapo vya mahakama, vyeti vya ndoa, ubatizo n.k.
  • Cheti halisi chenye jina lilikosewa ni lazima kirudishwe NECTA kwaajili ya mchakato wa marekebisho.

Hatua Za Kufuata Wakati wa Kufanya Maombi

  • Fungua tovuti (Website) ya NECTA (www.necta.go.tz)
  • Chagua na ubonyeze huduma mtandao (E-services)
  • Ingiza Nambari ya simu ili kupata nambari ya uthibitisho (code number)
  • Ingiza nambari ya uthibitisho (Code) uliyopokea kwenye simu yako (tarakimu nne [04])
  • Ingiza barua pepe yako.

Namna ya kufanya malipo kwa kutumia ‘Control Number’

  • Ingiza tena nambari yako ya simu
  • Ingiza tena anwani yako ya barua pepe
  • Ingiza majina ya mwombaji kama yalivyoandikwa kwenye cheti / Hati ya matokeo.
  • Chagua huduma (Correction of Names)
  • Tengeneza control number (Generate Bill).
  • Lipia ada ya marekebisho ya jina ya Tsh.35, 000/= (kwa cheti kimoja) kupitia benki au mitandao ya simu kwa kutumia ‘Control number’ uliyotengeneza.

Baada ya kufanya malipo

  • Bonyeza Marekebisho ya Majina (Correction of Names) na ufanye maombi (Apply/New).
  • Ingiza nambari ya simu ya mkononi na nambari ya malipo (Control Number).
  • Jaza fomu ya maombi mtandao (Online Application Form) kisha Wasilisha ombi kwa kubofya ‘Submit’.

Majibu Kwa Mteja
Baada ya marekebisho kufanyika, Hati ya Matokeo (Results Slip) au cheti kipya chenye marekebisho kitatumwa kwa mkuu wa shule au kwa mtahiniwa (endapo si mwanafunzi).

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags: ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *