MAGAZETI ya Leo Alhamisi 27 Machi 2025
MAGAZETI ya Leo Alhamisi 27 Machi 2025
Mahakama Kuu Masijala Ndogo ya Mbeya, imemuhukumu adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja jela, Hamphrey Ngogo, baada ya kumkuta na hatia ya kumuua mpenzi wake Faraja Shabani, bila kukusudia.
Katika kesi hiyo ya jinai ya mwaka 2023, hukumu yake imetolewa Machi 25, 2025 na Jaji Mussa Pomo na nakala yake kupatikana kwenye mtandao wa mahakama.
Awali Ngogo alishtakiwa kwa kosa la mauaji alilolitenda kinyume na kifungu cha 196 cha Kanuni ya Adhabu.
Ngogo wakati anatenda kosa hilo Septemba 2, 2022 katika eneo la Mkuyu kata ya Iganzo, mkoani Mbeya alikuwa na miaka 17.
Upande wa mashitaka ulieleza kuwa Ngogo alikiri kutenda kosa hilo na kuwa siku ya tukio alikwenda nyumbani kwa akina Faraja kwa lengo la kufanya naye mapenzi, ila marehemu hakuwa tayari ndipo alipomkaba shingo ili asipige kelele.
Ilielezwa kuwa licha ya kujaribu kumkaba marehemu aliendelea kupiga kelele, mshtakiwa akaenda kuchukua shoka na kumpiga nalo kichwani na baada ya kuona Faraja hazungumzi tena, alitoka nje na kukimbia.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
