MAGAZETI ya Leo Ijumaa 11 April 2025

Filed in Magazeti, Michezo by on April 11, 2025 0 Comments
     
MAGAZETI ya Leo Ijumaa 11 April 2025

MAGAZETI ya Leo Ijumaa 11 April 2025

MAGAZETI ya Leo Ijumaa 11 April 2025

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetanganza kufungua dirisha kwa wanachama wake wanaotaka kuwania udiwani, uwakilisha na ubunge katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.

Chama hicho tawala nchini Tanzania kimesema fomu za kuomba kuteuliwa kuwania nafasi hizo zitaanza kutolewa Mei 1-15, 2025.

Taarifa kwa umma iliyotolewa Alhamisi, Aprili 10, 2025 na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla imeelezea utaratibu kuwa wanachama wanaogombea nafasi ya ubunge au ujumbe wa Baraza la Wawakilishi watachukua na kurudisha fomu kwa Katibu wa CCM wa Wilaya inayohusika.

Makalla amesema wanachama wanaogombea nafasi za Viti Maalumu vya wanawake katika Bunge au Baraza la Wawakilishi, kupitia kundi la Umoja wa Wanawake (UWT) pamoja na makundi maalumu NGO, wafanyakazi, wasomi na wenye ulemavu watachukua fomu na kurudisha kwa Katibu wa UWT wa Mkoa unaohusika.

Amesema wanachama wanaogombea nafasi za Viti Maalumu vya wanawake katika Bunge au Baraza la Wawakilishi kupitia jumuiya ya Vijana wa chama hicho (UVCCM) watachukua na kurudisha fomu kwa Katibu wa UVCCM Mkoa unaohusika.

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *