MAGAZETI ya Leo Ijumaa 14 Machi 2025
MAGAZETI ya Leo Ijumaa 14 Machi 2025
Serikali kupitia Waziri wa Afya nchini imetangaza kumalizika kwa mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Marburg katika Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera.
Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Jenista Mhagama Machi 13, 2025 akisema mgonjwa wa mwisho aliyethibitika kuwa na virusi hivyo (MVD) aliripotiwa Januari 28, 2025 hivyo hadi kufikia Machi 11, 2025, ni siku 42 zinakuwa zimepita tangu kuwepo kwa mgonjwa huyo wa mwisho.
“Kitaalamu na kulingana na kanuni na taratibu za Shirika la Afya Duniani WHO, tumekidhi vigezo vya kutangaza rasmi kumalizika kwa mlipuko wa MVD. Hivyo basi, leo Machi 13, 2025, ninatangaza rasmi kumalizika kwa mlipuko wa MVD nchini,” amesema Mhagama.
Januari 20, 2025, Rais Samia Suluhu Hassan, alitangaza uwepo wa mlipuko wa ugonjwa wa Virusi vya Marburg mkoani Kagera, ambapo wagonjwa wawili walithibitika kuwa na maambukizi.
TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
