Magazeti ya Leo Ijumaa tarehe 7 Machi 2025
Magazeti ya Leo Ijumaa tarehe 7 Machi 2025
Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imetangaza gharama za usafirishaji wa mizigo ya haraka (Express Luggage) kati ya Guangzhou na Dar es Salaam au Zanzibar.
Gharama mpya, ambazo zilianza kutumika rasmi tarehe 1 Machi 2025, ni RMB 1,800 kwa kilo 32, ikiwa ni ongezeko la RMB 200 kutoka bei ya awali.
ATCL imesema kuwa gharama hizi bado ni nafuu ikilinganishwa na makampuni mengine ya ndege ambayo hutoza hadi RMB 2,000 kwa kilo 32. Tangu kuanza kutumia viwango vipya, ATCL imesafirisha mizigo 236 yenye uzito wa kilo 7,552.
“Ingawa kuna ongezeko la kidogo la gharama, huduma zetu bado zinabaki kuwa ushindani kwenye soko, tukizingatia usalama kwanza, ufanisi na ufikishaji wa mizigo kwa wakati,” alisema Sarah Reuben, Meneja Uhusiano na Mawasilino kwa Umma, ATCL.
Kwa upande mwingine ATCL imewashukuru wateja wake na kuwahimiza kufanya mawasiliano na kampuni hiyo iwapo wanahitaji taarifa yoyote kuhusu huduma ya usafirishaji wa mizigo ya haraka.
TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
