MAGAZETI ya Leo Jumanne tarehe 11 Machi 2025

Filed in Magazeti, Michezo by on March 11, 2025 0 Comments
     

MAGAZETI ya Leo Jumanne tarehe 11 Machi 2025

Kiungo Mshambuliaji wa Young Africans, Stephane Aziz Ki na beki wa Simba SC, Valentino Nouma wametemwa katika kikosi cha Burkina Faso kilichotangazwa kuitwa leo Jumatatu na kocha Brama Traore kwaajili ya michezo miwili ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2026.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Burkina Faso itakuwa nyumbani Machi 16 2025 kucheza mchezo wa tano wa makundi dhidi ya Djibouti kabla ya kusafiri kuifuata Guinea Bissau Machi 23.

Ikumbukwe kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 alikuwepo katika kikosi kilichocheza mechi za mwanzoni za michuano hiyo akicheza michezo mitatu na kutoa pasi iliyozaa bao.

Burkina Faso inashika nafasi ya tatu katika Kundi A ikivuna pointi tano katika michezo minne iliyocheza, nyuma ya Guinea Bissau yenye alama 6 na Misri inayoongoza kundi hilo ikiwa na pointi 10.

Kikosi kamili cha Burkina Faso kilichoitwa leo ni;

Makipa ni Kylian Nikiema, Hervé Koffi, Farid Ouédraogo.

Mabeki wakiwa ni; Issa Kabore, Steeve Yago, Edmond Tapsoba, Nasser Djiga Issoufou Dayo, Adamo Nagalo,Kouassi Guy Arsène na Mohamed Yabre.

Viungo ni; Memel Dao, Cedric Badolo Mohamed Zoungrana, Blati Toure Josue Tiendrebeogo, Saidou Simpore, Dramane Salou, Ishmaila Ouédraogo.

Washambuliaji ni; Franck Lassina Traore Dango Ouattara, Bertrand Traore, Hassane Bande, Mohamed Konate na Cyriaque Iri.

TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!