Magazeti ya Leo Jumanne tarehe 4 Machi 2025
Magazeti ya Leo Jumanne tarehe 4 Machi 2025
Soma hapa kurasa za Mbele za Magazeti ya Leo Jumanne tarehe 4 Machi 2025 Kupitia Habari Web Blog Habari Bila Mipaka.
Askari 260 wa Jeshi la Ulinzi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) waliokamatwa kwa kosa la kuwakimbia wapiganaji wa Kundi la M23 na kufanya uhalifu wa kivita mashariki mwa nchi hiyo, wamehukumiwa adhabu ya kifo.
Shirika la Habari la Reuters limeripoti Jumatatu Machi 3, 2025 kuwa kati yao, askari 55 wa FARDC walihukumiwa mahakamani eneo la Musienene Ijumaa ya Februari 28, 2025.
Zaidi ya askari 200 walitoroka baada ya wafungwa kuvunja gereza moja wakati wa uvamizi wa M23 uliosababisha Jeshi la FARDC kurudi nyuma huko Bukavu Februari 14.
Msemaji wa Kikosi cha Jeshi la FARDC linalopigana huko mashariki mwa DRC, Luteni Kanali Mak Hazukay, amesema kuwa wanajeshi walioshtakiwa wamelivunjia jeshi hilo heshima na kufanya ukatili unaoweza kuwafanya raia kuwasaidia waasi kusonga mbele.
Mashambulizi ya M23 tangu mwishoni mwa Desemba yameonekana kuwa hatari kwa vikosi vya Serikali ya Rais Felix Tshisekedi ikilinganishwa na mashambulizi ya yaliyofanywa na waasi hao takriban mwongo mmoja uliopita.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
