MAGAZETI ya Leo Jumapili 06 April 2025

Filed in Magazeti, Michezo by on April 6, 2025 0 Comments
     

MAGAZETI ya Leo Jumapili 06 April 2025

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza kurejea kwa huduma ya ununuzi wa tiketi za treni kupitia mtandao baada ya kukabiliwa na hitilafu ya mfumo wa malipo ya Serikali, maarufu kama Government Electronic Payment Gateway (GePG).

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Katika taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano wa TRC, Fredy Mwanjala shirika hilo limeeleza kuwa changamoto hiyo ilianza usiku wa kuamkia Aprili 5, 2025, na ilisababisha baadhi ya wasafiri kushindwa kupata namba za malipo (control number) kwaajili ya kununua tiketi za treni za kisasa (SGR).

“Shirika linaarifu umma kuwa hali ya upatikanaji wa tiketi kwa njia ya mfumo wa GePG imerejea kama kawaida,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

TRC imetoa pole kwa abiria wote waliokumbwa na usumbufu uliotokana na hitilafu hiyo ya muda mfupi na kuahidi kuendelea kuboresha huduma zake ili kuhakikisha huduma zinapatikana bila vikwazo.

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *