Magazeti ya Leo Jumapili tarehe 02 March 2025

Filed in Magazeti, Michezo by on March 2, 2025 0 Comments
     

Magazeti ya Leo Jumapili tarehe 02 March 2025

Selemani Salum Bwenzi ni miongoni mwa Wachezaji wanaofanya vizuri katika kikosi cha KenGold kutokana na uwezo anaoendelea kuuonyesha, baada ya kuchangia mabao sita ya Ligi Kuu hadi sasa, akifunga matano na kuasisti moja.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Bwenzi aliyejiunga na kikosi hicho dirisha dogo la January mwaka huu akitokea Mbeya Kwanza inayoshiriki Ligi ya Championship, ameelezea mengi, ikiwemo bao kali alilomfunga kipa wa Yanga, Djigui Diarra.

Nyota huyo anasema kuwa licha ya kufunga mabao matano ya Ligi Kuu Bara hadi sasa, ila bao bora kwake lililompa heshima kubwa ni lile la mbali alilomfunga kipa wa Yanga, Djigui Diarra, wakati KenGold ilipochapwa mabao 6-1, February 5, mwaka huu.

“Iliniuma sana kuona tunapoteza mchezo kwa idadi kubwa ya mabao lakini baada ya kufunga lile bao lilinipa heshima ambayo sikufikiria kama ingetokea, mapokezi yalikuwa makubwa na ndipo nilipoamini nyota yangu inaanza kung’aa upya,” anasema.

Bao la nyota huyo lilitokea baada ya Duke Abuya kuifungia Yanga bao la sita dakika ya 84 na wakati mpira huo unaanza katikati, alipiga shuti la moja kwa moja na kumshinda Diarra ambaye alionekana wazi amezidi mbele kidogo ya lango lake.

Anasema safari yake ya soka ilianzia mtaani maeneo ya Tandale Shule jijini Dar es Salaam na mtu ali-yemfanya kufika hapa alipo leo ni makocha waliojulikana kwa jina la Kisaga, akishirikiana na Mzee mwenzake, Simeni waliokuwa wanaishi wote.

“Ni miongoni mwa makocha ambao sitokaa niwasahau katika maisha yangu, walikuwa nguzo imara ya kunifikisha hapa nilipo leo, kwa sababu misingi yote ya soka walianza kunipa wao, kuanzia nidhamu ambayo ndio msingi wa jambo lolote,” anasema.

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *