MAGAZETI ya Leo Jumapili tarehe 9 Machi 2025

Filed in Magazeti, Michezo by on March 8, 2025 0 Comments
     

MAGAZETI ya Leo Jumapili tarehe 9 Machi 2025

Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel, amewataka Watanzania kuhamasishana kukata bima ya afya ili kuepuka changamoto za kugharamia matibabu wanapokumbwa na maradhi.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Akizungumza Jumamosi Machi 8, 2025, katika maadhimisho ya Siku ya Figo Duniani jijini Dar es Salaam, Dk Mollel amesema kuwa bima ya afya ni suluhisho la kudumu kwa changamoto za matibabu, hasa kwa magonjwa sugu kama figo, ambayo gharama zake ni kubwa.

“Bima ya afya ndiyo mwarobaini wa matatizo ya matibabu. Ili kujikinga na ugonjwa wa figo, tunapaswa kudhibiti kiwango cha sukari, shinikizo la damu na magonjwa mengine yanayoweza kuathiri figo. Lakini pia, sote tunapaswa kuwa mabalozi wa kuhamasisha ukataji wa bima ya afya,” amesema.

Katika maadhimisho hayo, Hospitali ya Saifee ilitoa huduma za uchunguzi wa afya bila malipo kwa wananchi, hatua iliyowezesha wengi wao kutambua hali zao za kiafya mapema.

Mwakilishi wa hospitali hiyo, Dk Abbas Essajee amesema wamebaini ongezeko la wagonjwa wa figo, hasa wenye umri wa kati ya miaka 30 hadi 45, jambo linaloashiria umuhimu wa tahadhari za kiafya mapema.

“Tunawahimiza watu kuchukua hatua za kulinda afya zao kwa kuzingatia mtindo bora wa maisha. Ni muhimu kunywa maji ya kutosha, kula chakula chenye lishe, kufanya mazoezi mara kwa mara na kuhudhuria uchunguzi wa afya kwa vipindi maalumu ili kugundua matatizo mapema,” amesema Dk Essajee.

TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!