MAGAZETI ya Leo Jumatano 26 Machi 2025

Filed in Magazeti, Michezo by on March 26, 2025 0 Comments
     

MAGAZETI ya Leo Jumatano 26 Machi 2025

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema kuwa Serikali imeanza taratibu za kuanzisha ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kuunganisha mikoa ya kaskazini.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Kadogosa ameyasema hayo Jumanne Machi 25, 2025 jijini Arusha alipokutana na Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda.

Kwa sasa reli hiyo ya kisasa inafanya kazi kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, huku ujenzi wa kutoka Dodoma hadi Mwanza ukiwa unaendelea.

Akizungumzia hatua hiyo mpya ya kujenga SGR na kuunganisha mikoa ya kaskazini, Kadogosa amesema: “Arusha ina maana kubwa sana, sio tu tunajenga reli ya SGR kuja huku lakini tuna sababu za kiuchumi, kuna madini ya soda pia ambayo ni uchumi mkubwa na machimbo yanaweza kuwepo zaidi ya miaka 100, lakini jambo jingine muhimu kwa Watanzania ni ujio wa bomba la mafuta kutoka Uganda kuja Tanga.”

Makonda amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa maono yake kwa Mkoa wa Arusha.

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *