Magazeti ya Leo Jumatano tarehe 05 Machi 2025
Magazeti ya Leo Jumatano tarehe 05 Machi 2025
Soma hapa Habari Kubwa Kwenye Kurasa za Mbele za Magazeti ya Leo tarehe 5 Machi 2025, Kurasa za Mbele Magazeti ya Leo Jumatano Machi 5, 2025.
Wakati dabi ukiwa ndio mchezo unaofuata kati ya timu hizo, kocha wa Yanga, Hamdi Miloud amewasifu Wachezaji wake kuonyesha ukomavu mkubwa dhidi ya Pamba, lakini amekuwa akijipa muda kwaajili ya Dabi ya Kariakoo.
Kikosi cha Yanga hicho kilikuwa na michezo miwili mfululizo ugenini kikicheza dhidi ya Mashujaa na Pamba Jiji, na kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 8-0 katika mechi zote mbili.
Mabingwa hao watetezi hadi sasa wameweka rekodi ya kucheza mechi 22 wakijizolea pointi 58 wakiongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.
Akizungumza Hamdi alisema amefurahishwa na kiwango cha wachezaji wake.
“Kwenye hizi mechi tano zilizopita baada ya sare dhidi ya JKT, wachezaji wangu walionyesha ukomavu mkubwa wakiendelea kufanya mabadiliko machache ninayoendelea kuwapa,” alisema.
“Kuhusu mchezo dhidi ya Simba, zinakwenda kukutana timu mbili bora msimu huu zinazoendelea kupishana juu ya msimamo. Nataka kukaa chini na kuwaza ni namna gani nitaingia tofauti kwenye mchezo huo mgumu. Lakini naamini wachezaji wangu watafanya kitu kikubwa, kwani Yanga tutaingia kivingine ili tupate ushindi,” alisema.
Yanga imeizidi Simba alama nne kileleni, huku wababe hao wa Jangwani wakiwa mbele kwa kucheza mechi 22 ilhali Simba wamecheza mechi 21.
Mabingwa hao mara tatu mfululizo wanaonyesha kujiamini kutokana na pointi za Simba wao kuwa chini, kwani hata akicheza mechi ijayo na hawezi kuwafikia.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
