MAGAZETI ya Leo Jumatano tarehe 12 Machi 2025
MAGAZETI ya Leo Jumatano tarehe 12 Machi 2025, haya hapa Magazeti ya Leo Jumatano tarehe 12 Machi 2025, Kurasa za Mbele za Magazeti ya Tanzania Leo Jumatano 12 Machi 2025.
Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, imefanya kikao chake maalum tarehe 10 Machi, 2025 jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Katika kikao hicho, Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imepokea na kujadili agenda kuu mbili kama zifuatazo:-
- Mapendekezo ya Marekebisho ya Kanuni za Uteuzi wa Wagombea Uongozi katika Vyombo vya Dola toleo la 2022 na
- Rasimu ya Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa 2025 – 2030.
Kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Kanuni za Uteuzi wa Wagombea Uongozi katika Vyombo vya Dola, Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imeridhia mapendekezo ya marekebisho ya Kanuni hizo.
Maeneo yaliyofanyiwa marekebisho ni kama ifuatavyo:-
- Mchakato wa uchujaji na uteuzi wa wagombea wa nafasi za ubunge, uwakilishi wa majimbo na udiwani wa kata/wadi.
- Mchakato wa uchujaji na uteuzi wa wagombea wa nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani wa viti maalum wanawake.
- Upanuzi wa wigo wa idadi ya wajumbe wa vikao vya chama na jumuiya zake watakaopiga kura za maoni.
Lengo la hatua hii ni kuimarisha misingi ya demokrasia, uwazi na kupanua uwakilishi wa wanachama wa CCM katika kuwapata wagombea wa nafasi za uongozi katika chaguzi za vyombo vya dola.
Utaratibu utakuwa kama ifuatavyo:-
Kwa upande wa wabunge wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) ngazi ya mikoa, kwa upande wa Tanzania Bara Mkutano Mkuu Maalumu wa UWT wa Mkoa, ambao utakuwa na wajumbe wafuatao :-
- Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa UWT wa Mkoa (Kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni za UWT).
- Wajumbe wote wa Kamati za Utekelezaji wa UWT za Wilaya.
- Wajumbe wote wa Kamati za Utekelezaji wa UWT za Kata.
Kwa upande wa Zanzibar Mkutano Mkuu Maalumu wa UWT wa Mkoa, utakuwa na wajumbe wafuatao :-
- Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa UWT wa Mkoa.
- Wajumbe wa Kamati za Utekelezaji za Wilaya.
- Wajumbe wa Kamati za Utekelezaji za Jimbo.
- Wajumbe wa Kamati za Utekelezaji za Kata/Wadi. Wajumbe wa Kamati za Utekelezaji za Matawi.
Kwa upande wa Jumuiya ya UVCCM na WAZAZI
Kura za maoni kwa waombaji nafasi za Ubunge/Uwakilishi wa viti maalumu wanawake kupitia Jumuiya ya UVCCM na WAZAZI zitapigwa na wajumbe wa Mikutano Mikuu Maalumu ya Taifa, kwa utaratibu ufuatao:-
Mikutano Mikuu ya Taifa ya UVCCM/WAZAZI itakua na wajumbe Wanawake tu; wajumbe hao ni kama wafuatao
- Wajumbe wote wanawake wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa UVCCM/WAZAZI.
- Wajumbe wote Wanawake wa Kamati za Utekelezaji za UVCCM/WAZAZI za Mikoa.
- Wajumbe wote Wanawake wa Kamati za Utekelezai za Wilaya UVCCM /Wazazi.
Ukomo wa viti maalum
Kuweka ukomo wa vipindi viwili vya miaka mitano kwa nafasi za ubunge/ uwakilishi na udiwani wa viti maalum wanawake. Ukomo huo utaanza kutumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2030.
Vilevile, Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imepitisha Kauli Mbiu rasmi kwa ajili ya kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2025 isemayo; “KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE”
Kauli mbiu hiyo inaakisi dhamira ya Chama ya kuendeleza juhudi za ujenzi wa Taifa lenye maendeleo jumuishi, mshikamano wa kitaifa na ustawi wa watu wenye kujali UTU.
TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
