MAGAZETI ya Leo Jumatatu 17 Machi 2025
MAGAZETI ya Leo Jumatatu 17 Machi 2025
Baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kutangaza kuufungia Uwanja wa Benjamin Mkapa, Serikali ya Tanzania imeeleza kuwa ukaguzi wa CAF ulifanyika takribani wiki mbili zilizopita, mara baada ya mchezo kati ya Simba na Azam Februari 24, 2025.
Wakati wa ukaguzi huo, uwanja ulikuwa umekatwa nyasi hadi chini kabisa, hali iliyosababisha wakaguzi wa CAF kutoa maelekezo ya kurekebisha eneo la kuchezea (pitch), ambapo Marekebisho hayo tayari yamefanyika.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, akizungumza Machi 16, 2025, amesema kuwa ana imani kuwa mechi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simba na Al Masry itachezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Aprili 9, mwaka huu, endapo wakaguzi wa CAF watakaporejea Machi 20, 2025, na kuthibitisha kuwa uwanja huo unakidhi vigezo vya kuandaa mchezo huo.
Katika hatua nyingine, Tanzania haitokuwa na refa katika Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji walio chini ya umri wa miaka 17 (Afcon U17) 2025 zitakazofanyika Morocco baadaye mwezi huu.
Katika orodha ya mwisho ya marefa 45 walioteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuchezesha fainali hizo mwaka huu, hakuna jina la refa wa kati wala msaidizi kutoka Tanzania.
Kama ilivyo kwa Tanzania, Kenya nao hawajabahatika kuwakilishwa na refa kwenye fainali hizo huku Rwanda, Sudan, Uganda na Djibouti zikipata fursa hiyo muhimu kwa upande wa nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).
Orodha ina marefa 17 wa kati, 18 wa pembeni na 10 ambao wataongoza teknolojia ya video ya usaidizi kwa marefa (VAR).
Marefa 17 wa kati ni Vincent Kabore (Burkina Faso), Patience Rulisa na Alinę Umutoni (Rwanda), Barbosa Lenine (Cape Verde), Fleury Moukagny (Gabon), Asamoah Collins (Ghana), Josiano Elivas (Madagascar), Abdulwahid Huraywida (Libya), Hamza Elfariq (Morocco), Sadou Ali (Niger), Keren Yocette (Shelisheli), Lucky Kasalirwe (Uganda), Brighton Chimene (Zimbabwe), Karboubi Bouchra (Morocco), Amedome Vincentia (Togo) na Ghada Mehat (Algeria).
Marefa wasaidizi 18 ni Alao Salim (Benin), Sawadogo Levy (Burkina Faso), Dirir Robleh (Djibouti), Mwanya Mbilizi (DR Congo), Birama Kone (Mali), Abdessamad Abertoune (Morocco), Ousmana Aboubakar (Niger), Didier Ishimwe na Alice Umutesi (Rwanda) na Luis Ferreira (Sao Tome).
Wengine ni Cledwin Baloyi (Afrika Kusini), Jermoumi Fathia (Morocco), Nancy Kasitu (Zambia), Nafissatou Yekini (Benin), Asma Feriel (Algeria), Hannah Moses (Liberia), Tabara Mbodj (Senegal) na Mireille Kanjinga (DR Congo).
Hiyo ni mara ya kwanza kwa Tanzania kutokuwa na refa kwenye fainali za Afcon U17 baada ya kufanikiwa kupeleka marefa katika awamu tatu mfululizo zilizopita za mashindano hayo yanayofanyika kila baada ya miaka miwili.
Awamu iliyopita, refa aliyeiwakilisha Tanzania alikuwa ni Ahmed Arajiga na kabla ya ya hapo mwaka 2019, refa wa kati Jonesia Rukyaa na msaidizi, Mohamed Mkono walichezesha fainali hizo.
TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags: Habari Kubwa kwenye Magazeti ya Leo Jumatatu tarehe 17 Machi 2025, Haya hapa Magazeti ya Tanzania Leo Jumatatu tarehe 17 Machi 2024, Kurasa za Mbele za Magazeti ya Tanzania Leo Jumatatu 17 Machi 2025, MAGAZETI ya Leo Jumatatu 17 Machi 2025, Magazeti ya Tanzania Leo tarehe 17 Machi 2025, Mezani Leo Magazeti ya Jumatatu tarehe 17-03-2025.