MAGAZETI ya Leo Jumatatu tarehe 10 Machi 2025
MAGAZETI ya Leo Jumatatu tarehe 10 Machi 2025
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (Zura) imesema kuwa bei za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa/ndege zimepanda kwa sababu ya kuongezeka gharama za uingizaji wa nishati hiyo nchini.
Akitoa taarifa za mabadiliko hayo kuanzia Jumapili, Machi 9, 2025, Kaimu meneja kitengo cha uhusiano Zura, Shara omar Chande amesema bei hizo zimepanda kutokana na ongezeko la bei katika soko la dunia.
Lita ya mafuta ya petroli itauzwa kwa Sh2, 939 ikilinganishwa na Sh2, 819 za mwezi uliopita, ikiwa ni ongezeko la Sh120 sawa na asilimia 4.25.
Mafuta ya dizeli lita moja itauzwa Sh3, 135 ikilinganishwa na Sh2,945 tofauti ya Sh190 sawa na asilimia 6.45 huku mafuta yakiongezeka kwa Sh77 kutoka Sh2,423 hadi Sh2,500 sawa na asilimia 3.17.
“Mafuta ya taa yataendelea kuuzwa kwa bei ileile ya Sh3, 200,” amesema.
Ametaja sababu nyingine ni uingizaji wa mafuta na kuongezeka kwa wastani wa thamani ya dola ya Marekani ikilinganishwa na shilingi ya Tanzania.
TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
