MAGAZETI ya Tanzania Leo Alhamisi 30 January 2025
MAGAZETI ya Tanzania Leo Alhamisi 30 January 2025
Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, Toleo la 2023, inayolenga kuleta mageuzi makubwa na ya kipekee katika sekta ya elimu nchini.
Miongoni mwa mageuzi yaliyopo kwenye sera hiyo ni kufundishwa kwa somo la Tehama, mafunzo ya ufundi stadi kuanzia Elimu ya msingi, na matumizi ya akili mnemba (AI).
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema hayo Jumatano ya January 29, 2025, alipokuwa akizungumzia uzinduzi wa sera hiyo, utakaofanyika Ijumaa, January 31, 2025, jijini Dodoma.
Msigwa, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, amesema lengo la kufanyiwa mapitio hayo ya sera ni kuwafanya wanafunzi kuwa na umahiri na ujuzi unaoakisi mahitaji kitaifa na kimataifa, ili kushindana na kushiriki kikamilifu kwenye soko la ajira duniani.
TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
