Magazeti ya Tanzania Leo Alhamisi February 20, 2025
Magazeti ya Tanzania Leo Alhamisi February 20, 2025
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ameiagiza Wizara ya Katiba na Sheria kuongeza kasi ya kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kuandika na kutunza wosia pamoja na kugawa mirathi kwa mujibu wa sheria ili kupunguza migogoro ya kijamii.
Majaliwa ametoa agizo hilo Jumatano February 19, 2025 wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia mkoani Lindi.
“Watu wengi hawaandiki wosia, hivyo naomba wananchi wajitahidi kufanya hivyo ili kuepusha changamoto ndani ya familia,” amesema.
“Niwaombe wakuu wa wilaya kutoa ushirikiano kwa viongozi watakao kuja kutoa msaada wa kisheria, hasa kwenye migogoro ya wosia, ardhi pamoja na migogoro ya kifamilia,” amesema Majaliwa.
Katika hotuba yake, Waziri Mkuu pia aliwataka viongozi wa dini na kimila kuendelea kuhubiri kuhusu upendo, mshikamano na maadili mema kuanzia ngazi ya familia ili kulinda amani na umoja wa jamii.
Aidha, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha na kugharamia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, ambayo kufikia Mei mwaka huu itakuwa imefanyika katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani. Kampeni hiyo inalenga kusaidia wananchi kutatua changamoto za kisheria bila gharama yoyote.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
