Magazeti ya Tanzania Leo Ijumaa February 21, 2025
Magazeti ya Tanzania Leo Ijumaa February 21, 2025
Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi (ARV) zinapatikana bure kwa wagonjwa wote nchini.
Dk Mollel ametoa kauli hiyo Alhamisi ya February 20, 2025, wakati akishiriki katika uzinduzi wa awamu ya tatu ya Mradi wa Timiza Malengo uliofanyika mkoani Lindi uliozinduliwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Ummy Deriananga, kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
“Serikali itaendelea kufanya kila juhudi kuhakikisha kwamba huduma za afya zinawafikia Watanzania wote bila ubaguzi ikiwa ni pamoja na dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKimwi (ARV) zaidi ya Sh48 bilioni imewekezwa kuboresha miundombinu ya afya, jambo la msingi ni wananchi kujenga utamaduni wa kupima afya ili kuepuka magonjwa,” amesema Dk Mollel.
Mradi wa Timiza Malengo, unaotekelezwa katika halmashauri 36 za mikoa 10, unalenga kuboresha huduma za afya, hasa vijijini.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
