Magazeti ya Tanzania Leo Jumamosi 15 February 2025
Magazeti ya Tanzania Leo Jumamosi 15 February 2025
Serikali imetaja mkakati wa ukarabati wa meli katika Ziwa Tanganyika na kuwa mwezi ujao (March) ujenzi wa meli ya Mv Sangara utakuwa umekamilika.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile ametoa kauli hiyo bungeni Dodoma February 14, 2025, kuwa Serikali ilishaanza mkakati wa ukarabati wa meli zinazotoa huduma katika Ziwa Tanganyika.
Kihenzile alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Bupe Mwakang’ata ambaye ameuliza Serikali ina mpango gani wa kukarabati meli katika Ziwa Tanganyika.
Amesema ukarabati wa meli ya Mv Liemba ulianza July 13, 2024 baada ya mkandarasi kulipwa malipo ya awali ya dola 1.9 kati ya Dola 13 milioni. zinazotakiwa kama sehemu ya malipo ya mradi mzima.
Kwa mujibu wa naibu waziri huyo, mkataba wa mradi huo utadumu kwa kipindi cha miezi 24, hivyo unatarajia kukamilika July 13, 2026.
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limemkamata mtu mmoja anayejifanya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), akiwa na sare za jeshi hilo.
Mtu huyo aliyefahamika kwa jina la Emmanuel Mapana (24), mkazi wa Mtaa wa Sima mjini Bariadi, alikutwa na sare zinazofanana na za jeshi hilo, zikiwa na cheo cha luteni.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Edith Swebe, mtuhumiwa amekamatwa na kikosi kazi cha kupambana na uhalifu na wahalifu mkoani humo Ijumaa February 14, 2025 saa 6:30 mchana.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa mtuhumiwa amekutwa kwenye gari na baada ya upekuzi amekutwakombati hizo, mkanda wa JWTZ na kompyuta mpakato moja.
Polisi wamesema Mapana alikuwa akitafutwa muda mrefu na jeshi hilo kwa kosa la kujifanya mtumishi wa Serikali.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
