Magazeti ya Tanzania Leo Jumamosi February 22, 2025

Filed in Michezo by on February 22, 2025 0 Comments
     

Magazeti ya Tanzania Leo Jumamosi February 22, 2025

Rais Samia Suluhu Hassan amewaasa wanawake nchini kutotumia elimu wanayoipata kuvuruga familia na jamii badala yake wahakikishe inawanufaisha wao, familia zao, na jamii kwa ujumla.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Akizungumza, Ijumaa, February 21, 2025, katika hafla ya kuadhimisha miaka 10 ya Programu ya Mwanamke Kiongozi, ambayo pia ilihusisha mahafali ya wahitimu takribani 110 wa programu hiyo, Rais Samia alisema:

“Ndugu zangu, tunasema ukimuelimisha mwanamke, umeelimisha jamii. Kwa hiyo, mnaohitimu na mliotangulia, nendeni mkawe chachu katika jamii. Elimu mnayopata na stadi za uongozi mnazopewa zikainufaishe jamii, familia na Taifa kwa ujumla. Haitegemewi kuwa usomi au nafasi ya kiuongozi unayoipata mwanamke iwe sababu ya kuvuruga familia au kuharibu watoto wake. Elimu na nafasi ya uongozi zisitufanye tukasahau wajibu wetu wa kijamii wa malezi na makuzi ya watoto wetu,” amesema Rais Samia.

Programu ya mwanamke kiongozi inalenga kuwawezesha wanawake kupata mafunzo ya uongozi, ushawishi, na usimamizi wa rasilimali kwa lengo la kukuza ushiriki wao katika nafasi mbalimbali za uongozi nchini.

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags: ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *