MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumanne 04 January 2025

Filed in Magazeti by on February 3, 2025 0 Comments
     

MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumanne 04 January 2025

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Felix Tshisekedi, na Rais wa Rwanda, Paul Kagame, wanatarajiwa kukutana Jumamosi ya tarehe 8 February 2025, jijini Dar es Salaam kwaajili ya kujadili mgogoro unaoendelea DRC.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Akitoa taarifa hiyo Jumatatu ya February 3, 2025, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Rais wa Kenya, William Ruto, amesema mkutano huo utahusisha marais wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (Sadc) na EAC.

“Rais Samia Suluhu Hassan amekubali kwa ukarimu kuandaa mkutano huo kujadili hali ya Mashariki mwa DRC,” amesema Rais Ruto.

Ruto ameongeza kuwa Rais Tshisekedi wa DRC na Rais Paul Kagame wa Rwanda ni miongoni mwa waliothibitisha kuhudhuria mkutano huo utakaotanguliwa na mkutano wa mawaziri Ijumaa ya February 7, 2025.

Pia, amesema kuwa wengine waliothibitisha kushiriki ni pamoja na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, na Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia.

Mkutano huo wa dharura unafanyika wakati DRC ikiishutumu Rwanda kuhusika na mgogoro unaoendelea nchini humo ukiongozwa na waasi wa M23, huku Rwanda nayo ikiishutumu DRC kutaka kuipindua Serikali yake.

TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!