Magazeti ya Tanzania Leo Jumanne 11 February 2025
Magazeti ya Tanzania Leo Jumanne 11 February 2025
Serikali ya Tanzania imeeleza mikakati mitano inayofanywa katika kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana nchini na namna kumudu ushindani kwenye soko la ajira.
Kauli hiyo inakuja siku chache baada ya February 5, 2025 wakati wa Sherehe za kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan kusema kuwa Serikali inaendelea kushughulikia suala la changamoto hiyo kwa kubuni vitu mbalimbali ambavyo vinaweza kuwakwamua kiuchumi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amesema hayo February 10, 2025 bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Mpendae (CCM), Toufiq Turky aliyehoji kuna mpango gani wa kuwandaa vyema vijana waweze kushindana katika soko la ajira ndani na nje ya Tanzania ili kukabiliana na upungufu wa ajira nchini.
Akijibu swali hilo, Waziri ametaja mipango ya Serikali katika kuwaandaa vijana ili kumudu ushindani katika soko la ajira ndani na nje ya nchi.
Ridhiwani amesema kuwa, mipango hiyo ni pamoja na kubuni na kutekeleza programu maalumu zinazowawezesha vijana kujifunza kwa vitendo kupitia sekta zinazozalisha ajira kwa wingi kama vile sekta ya kilimo kupitia programu ya Jenga Kesho iliyobora (BBT), ujasiriamali, na madini kupitia Programu ya Mining for a better Tommorrow (MBT).
Pia, amesema kufanya maboresho ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Tolea la Mwaka 2023 ambayo yanasisitiza mafunzo kwa kuandaa wataalamu.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
