Magazeti ya Tanzania Leo Jumanne 18 February 2025
Magazeti ya Tanzania Leo Jumanne 18 February 2025
Ripoti ya kitabibu kutoka Hospitali ya Gereza la Isanga iliyopo mkoani Dodoma imeonesha mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya mauaji ya mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, Padri Elipidius Rwegoshora ana akili timamu.
Mbali na Padri Rwegoshoro wa Kanisa Katoliki, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya mauaji ya kukusudia dhidi ya mtoto, Asimwe Novath ni baba mzazi wa mtoto (Asimwe).
Novath Venant, Nurdini Amada Masudi, Ramadhani Selestine,Rweyangira Burukadi Alphonce,Dastan Bruchard,Faswiu Athuman, Gozbert Alikad, Desdery Everist.
Ripoti hiyo, imesomwa leo Jumatatu Februari 17, 2025 na Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, wakati kesi hiyo ya mauaji namba 25513/2024, ilipoitwa kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali (PH).
Jaji wa Mahakama hiyo, Gabriel Malata aliyesoma ripoti hiyo, amesema amepokea ripoti yenye kumbukumbu namba/11927/2024 Desemba 16, 2024 iliyosainiwa na Dk Enock Changarawe kuwa mtuhumiwa huyo hana tatizo la afya ya akili wala dalili zake.
Katika hatua nyingine, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, ameagiza Jeshi la Polisi kufanya operesheni maalumu ya kudhibiti na kukomesha vitendo vya utapeli wa mtandaoni pamoja na wizi wa simu.
Ametoa agizo hilo leo, Jumatatu, Februari 17, 2025, alipotembelea Maabara ya Uchunguzi wa Makosa ya Kimtandao katika Kamisheni ya Uchunguzi wa Sayansi ya Jinai, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Bashungwa, takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonyesha kuwa mikoa ya Rukwa, Morogoro, Mbeya, na Dar es Salaam inaongoza kwa matukio ya utapeli wa mtandaoni, huku baadhi ya maeneo kama Ifakara yakitajwa kuwa kitovu cha uhalifu huo. Amesema wahalifu hao wanashirikiana kati ya mkoa mmoja na mwingine, hali inayohitaji hatua madhubuti za kiuchunguzi na kiusalama.
Amesema Serikali inachukua hatua za kuhakikisha Jeshi la Polisi linakuwa na vifaa na mifumo ya kisasa ya uchunguzi wa makosa ya kimtandao ili kuimarisha utendaji wake.
Aidha, ameagiza Jeshi hilo kushughulikia kwa haraka malalamiko ya wananchi kuhusu ucheleweshaji wa upelelezi wa simu zilizoibiwa, hali inayowafanya wahalifu kuepuka mkono wa sheria.
Kwa upande wake, Kamishna wa Uchunguzi wa Sayansi ya Jinai, Shabani Hiki, amesema kamisheni hiyo inaendelea kuboresha mifumo yake ya uchunguzi wa makosa ya mtandaoni.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
