MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumanne 25 February 2025
MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumanne 25 February 2025
Hussen Bundala ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake na watu wanaodaiwa kuwa ni watoto wake.
Kikongwe huyo, mkazi wa Kitongoji cha Ihanamilo kilichopo kata ya Nyamtukuza, Wilaya ya Nyanghwale mkoani Geita, aliuawa February 5, 2025.
Kufuatia mauaji hayo ambayo chanzo chake hakijajulikana, Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linawashikilia watoto watatu wa kikongwe huyo, wakituhumiwa kuhusika na mauaji hayo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, February 24, 2025, kikongwe huyo aliuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu za kichwani, usoni na shingoni.
Katika taarifa yake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo amewataja waliokamatwa kuwa ni Yombo Bundala (75) Makame Bundala (53) na Shija Bundala (50).
Kamanda Jongo amesema kuwa bado uchunguzi wa tukio hilo unaendelea kwa kushirikiana na vyombo vingine vya uchunguzi na uchunguzi ukikamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
