MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumanne tarehe 28 January 2025
MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumanne tarehe 28 January 2025
Wanafunzi saba wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Businda, iliyopo wilayani Bukombe, Mkoa wa Geita, wamefariki Dunia na wengine 82 kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi wakiwa darasani.
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Paskas Muragili, amesema kuwa tukio hilo limetokea leo Jumatatu, January 27, 2025, akieleza kuwa miongoni mwa majeruhi 82, wawili wana hali mbaya.
“Wakiwa darasani wakati mvua inanyesha, ilipiga radi na saba wamepoteza maisha. Kwa muonekano, sita ni wavulana na mmoja ni msichana, lakini bado tunafuatilia kujua majina yao kwani mimi sijaingia kwenye mochwari.
“Bado hatujawatambua waliopoteza maisha, lakini baadhi ya majeruhi tayari wameongea na kutuambia majina yao. Kadri hali inavyoendelea, tutapata taarifa rasmi,” ameongeza.
Mkuu huyo wa wilaya amesema kwamba, baada ya tukio hilo, madaktari walifika haraka shuleni hapo.
Hilo ni tukio la tatu kutokea mkoani Geita. Oktoba 18, 2019, wanafunzi 39 wa Shule ya Msingi Ihumilo, wilayani Geita, walijeruhiwa kwa kupigwa na radi, na Oktoba 17, 2018, wanafunzi sita wa Shule ya Msingi Emaco Vision walifariki dunia na wengine 23 kujeruhiwa kwa kupigwa na radi wakiwa darasani.
TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags: MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumanne tarehe 28 January 2025