Magazeti ya Tanzania Leo Jumapili 16 February 2025
Magazeti ya Tanzania Leo Jumapili 16 February 2025
K
iungo Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Stephane Azizi Ki amelipa mahari ya ng’ombe 30 kwa mwanamitindo Hamisa Mobetto.
Mahari hayo yametolewa Jumamosi, February 15, 2025 katika hafla iliyofanyika viwanja vya Gofu Lugalo, Jijini Dar es Salaam.
Mahari hiyo imekabidhiwa na Rais wa Yanga, Mhandisi Hersi Said, kwa niaba ya baba mzazi wa Aziz Ki, ambapo nyota huyo aliongozana na baadhi ya wachezaji wenzake wa Yanga.
Wachezaji waliohudhuria hafla hiyo ni Pacome Zouzoua, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Kibwana Shomari pamoja na Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ali Kamwe.
Kwa upande wa Hamisa yeye aliingia ukumbini na meneja wake Paul Mangoma huku warembo 15 wakitangulia mbele wakiwa wamevaa sare huku wakicheza.
Siku moja baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania masjala kuu ya Dodoma kuamuru kuitwa kortini wachezaji watatu wa Singida Black Stars, ili kujibu madai dhidi yao katika kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Wakili Peter Madeleka, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imethibitisha kwamba nyota hao wamesajiliwa kama wachezaji wa ndani.
Amri ya mahakama ilitolewa baada ya wachezaji hao Emmanuel Keyekeh, raia wa Ghana, Josephat Bada (Ivory Coast) na Mohamed Damaro Camara (Guinea) kutotokea mahakamani katika kesi dhidi yao ilipotajwa mbele ya Jaji Evaristo Longopa, wanakoshtakiwa kwa kupata uraia wa Tanzania kinyume cha utaratibu.
Lakini katika mahojiano, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Almas Kasongo, amesema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kina lakini wanaheshimu maamuzi ya taasisi yenye mamlaka ya uraia.
Aidha, amesisitiza kuwa uraia na usajili wa mchezaji ni mambo mawili tofauti, na kwamba mchakato wa usajili unazingatia vigezo vyake maalum.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
