Magazeti ya Tanzania Leo Jumapili 23 February 2025
Magazeti ya Tanzania Leo Jumapili 23 February 2025
Jeshi la Polisi limesema video inayosambaa ikimuonesha dereva bodaboda akikamatwa kwa nguvu katika eneo la Maili Moja, Kibaha mkoani Pwani ni askari walikuwa wanamkamata mhalifu ambaye alikaidi.
Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi February 22, 2025 katika kurasa zao za mitandao ya kijamii zimesema kuwa kijana huyo anatuhumiwa kufanya uhalifu kwa kutumia pikipiki maarufu ‘vishandu’.
“Picha hii mjongeo iliyopo kushoto inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na watu mbalimbali kutoa maoni yao ni tukio la ukamataji lililofanywa na askari Polisi Februari 20, 2025 katika eneo la Maili Moja, Mkoa wa Pwani.
“Mtuhumiwa huyo Rajabu Hassan alikuwa anatafutwa kutokana na tuhuma mbalimbali za kujihusisha na matukio ya uporaji kwa kutumia pikipiki ikiwa imekunjwa namba za usajili (plate number) na wakati mwingine ikiwa haina namba ya usajili kwa jina maarufu Vishandu,” imeeleza taarifa hiyo.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
