MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumapili 26 January 2025

Filed in Magazeti by on January 26, 2025 0 Comments
     

MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumapili 26 January 2025

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema kwasababu za kiusalama wale wanaotumia vyombo vya moto kama pikipiki za magurudumu mawili (bodaboda) na magurudumu matatu (bajaji) vyombo hivyo havitaruhusiwa kuingia katikati ya Jiji la Dar Es Salaam kufuatia Tanzania kuwa Mwenyeji wa Mkutano wa Nishati ambao Wakuu wa Nchi (Rais) kadhaa na
Mawaziri wa Fedha na Nishati wa Afrika watashiriki mkutano huo utakaofanyika Jijini Dar es salaam kuanzia January 27, 2025 hadi January 28,2025.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Muliro Jumanne amesema vyombo hivyo havitaruhusiwa kuingia katikati ya Jiji kwa muda ambao umetajwa wakati Wageni hao wakiwa bado wapo na wameshauriwa na kuelekezwa daraja la Salender kwa Watumiaji wa barabara ya Ally Hassani Mwinyi

Kwa barabara ya Morogoro wataishia Jangwani, kwa barabara ya Kawawa kutokea Magomeni wataishia Kigogo sambusa, kwa barabara ya Uhuru kutokea Buguruni wataishia llala Boma, kwa barabara ya Nyerere kutokea Airport na Veta wataishia taa za Veta na kwa barabara ya Kilwa wataishia Mivinjeni na kufuatia ugeni huo baadhi ya barabara zitafungwa kwa muda kupisha misafara ya Viongozi.

“Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linatoa wito kwa wananchi kufuata utaratibu huu na Jeshi la Polisi litajitahidi kuzisimamia hizo njia
mbadala ili kupunguza msongamano kwa kadri itakavyowezekana”

TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!