Magazeti ya Tanzania Leo Jumatano 19 February 2025

Filed in Magazeti by on February 18, 2025 0 Comments
     

Magazeti ya Tanzania Leo Jumatano 19 February 2025

Pacha waliotenganishwa nchini Saudi Arabia, Hussein na Hassan Amir (3) wameruhusiwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na wanatarajiwa kurejea Igunga, mkoani Tabora kesho baada ya kupata eneo la kuishi.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Pacha hao wanatarajiwa kwenda kuishi katika nyumba iliyotafutwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, wakati wakisubiri nyumba inayojengwa kukamilika.

Akizungumza na vyombo vya habari Jumanne, February 18, 2025, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila, Dk Julieth Magandi amesema watoto hao wanaruhusiwa baada ya matibabu ya miaka mitatu na miezi mitano.

Dk Magandi ametoa shukurani zake kwa Hospitali ya Saudi Arabia na serikali ya nchi hiyo iliyowezesha upasuaji wa saa 16 wa kuwatenganisha watoto hao uliofanyikwa kwa mafanikio makubwa.

Pacha hao walifanyiwa upasuaji wa kuwatenganisha uliochukua saa 16, October 2023 Saudi Arabia na kisha kurejea Muhimbili kwa ajili ya uangalizi na matibabu zaidi.

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *