MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumatano 26 February 2025
MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumatano 26 February 2025
Kwa mara nyingine Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la uwepo wa upepo mkali na mawimbi makubwa katika pwani ya kaskazini mwa Bahari ya Hindi.
Kwa takribani wiki moja sasa TMA imekuwa ikitoa angalizo kuhusu hali hiyo ikieleza kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni wastani.
Kwa mujibu wa taarifa ya hali mbaya ya hewa kwa siku tano, TMA imetoa angalizo la upepo mkali kuanzia February 25, 2025 hadi Alhamisi February 27.
“Angalizo la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili, limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya Kaskazini mwa Bahari ya Hindi,” imesema taarifa hiyo.
Mikoa inayotajwa kwa February 25 ni Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba.
Kwa February 26 na 27, TMA imetoa angalizo hilo kwa maeneo ya ukanda wa pwani kaskazini mwa Bahari ya Hindi mikoa ya Tanga, Dar es Salaam na Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
