Magazeti ya Tanzania Leo Jumatatu 10 February 2025

Filed in Magazeti by on February 9, 2025 0 Comments
     

Magazeti ya Tanzania Leo Jumatatu 10 February 2025

Barabara ya Sam Nujoma, jijini Dar es Salaam ilipewa jina hilo la Rais wa kwanza na Baba wa Taifa la Namibia, Samuel Daniel Shafiishuna Nujoma miaka ya 1980, lengo likiwa kuenzi harakati za mpigania uhuru huyo.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Nujoma kama alivyopenda kuitwa amefariki dunia leo Jumapili Februari 9, 2025, akiwa na miaka 95 akiacha alama nchini kwake Namibia, Afrika na duniani.

Kabla ya kuwa Rais wa Taifa hilo, nchini Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere alienzi harakati zake na kwa heshima, aliipa moja ya barabara za jijini Dar es Salaam jina la mwanamema huyo mashuhuri wa Afrika, ambaye leo amelala usingizi wa umauti.

Barabara hiyo ni ile inayotoka Mwenge kuanzia kwenye makutano na Barabara ya Bagamoyo hadi Ubungo maarufu Barabara ya Sam Nujoma ikiwa ni ufupisho wa jina lake la Samuel na la baba yake, Nujoma.

Mmoja wa watu wanayoilewa vema historia ya Jiji la Dar es Salaam, Sheikh Khamis Mataka anasema awali barabara hiyo ilikuwa ikiitwa barabara ya Mlimani kabla ya kubadilishwa kuwa Sam Nujoma.

TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *