MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumatatu 24 February 2025

Filed in Magazeti by on February 23, 2025 0 Comments
     

MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumatatu 24 February 2025

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Kuu Tanzannia (TPLB) imefuta adhabu ya kadi nyekundu (Red Card) kwa mchezaji wa Namungo, Derick Mukombozi aliyoadhibiwa na mwamuzi wa mchezo dhidi ya Simba.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Kamati imefikia maamuzi hayo baada ya kujiridhisha kuwa maelezo yaliyopo kwenye ripoti ya mwamuzi hayana ushahidi wa kutosha unaoendana na marejeo ya picha mjongeo kuwa Mukombozi alistahili kadi nyekundu.

Ikumbukwe kuwa Namungo ilipoteza mchezo huo kwa mabao 3-0 katika Uwanja wa Majaliwa Lindi. Pia mwamuzi alitoa penalti tatu katika mchezo huo.

Katika hatua nyingine, Vatican imesema Papa Francis, ambaye amelazwa hospitalini kwa zaidi ya wiki moja bado yuko katika hali ya ‘mahututi’ huku akipatwa na changamoto katika mfumo wa upumuaji, ‘pumu.’

“Asubuhi ya leo (jana), Papa Francis alipata changamoto ya kupumua kwa kiwango kikubwa, ambayo pia ilihitaji matumizi ya oksijeni kwa kiwango cha juu,” iliandika taarifa ya Vatican kuhusu hali ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki aliyelazwa Hospitali ya Gemelli mjini Roma.

Taarifa hiyo pia imesema, ingawa Papa Francis alikuwa macho huku akitumia kiti cha kusukumwa kwa mikono, alipoketi kwenye kiti hicho alidai kupata maumivu makali mwilini mwake zaidi ya Ijumaa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kiongozi huyo wa kiroho pia aliongezewa damu ili kutibu tatizo la anemia lililomkumba.

Mapema Jumamosi, Vatican ilisema atabaki hospitalini baada ya kukumbwa na nimonia na hataweza kuongoza sala ya kila wiki ya Angelus, ikiwa ni mara ya tatu tu katika karibu miaka 12 ya huduma yake kama Papa.

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *