MAJINA 1520 ya Wafanyabiashara wanaorejeshwa Soko la Kariakoo

Filed in Habari by on February 2, 2025 0 Comments
     
MAJINA 1520 ya Wafanyabiashara wanaorejeshwa Soko la Kariakoo

MAJINA 1520 ya Wafanyabiashara wanaorejeshwa Soko la Kariakoo

MAJINA 1520 ya Wafanyabiashara wanaorejeshwa Soko la Kariakoo

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Menejimenti ya Shirika la Masoko ya Kariakoo ipo katika hatua za mwisho za kurejea kwenye shughuli zake katika Soko kuu la Kariakoo baada ya kukamilika kwa ujenzi na Ukarabati wa soko.

Ili shughuli hizo ziweze kurejea, Shirika linatangaza kwa Umma orodha ya Wafanyabiashara 1,520 ambao wamehakikiwa na Kamati iliyoundwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.

Kila mfanyabiashara atakayeona jina lake katika orodha hii, anatakiwa kufika katika Ukumbi wa Anatoglo kuanzia siku ya Jumatatu ya tarehe 03.02.2025 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi siku ya Ijumaa ya tarehe 07.02.2025 kwaajili ya kujisajili kwa kujaza fomu na kufuata taratibu zinginezo za kiupangaji.

Mfanyabiashara anakumbushwa kufika akiwa na kitambulisho cha Taifa na namba ya Mlipakodi (TIN).

Hivyo, wafanyabiashara wenye madeni mnakumbushwa kulipa madeni yenu mnayodaiwa na Shirika ikiwa ni moja ya taratibu za kurejeshwa kabla hujapatiwa eneo la biashara.

Katika taarifa hiyo wafanyabiashara zaidi ya 366, hawataruhusiwa kurudi sokoni hapo hadi watakapolipa madeni waliokuwa wanadaiwa na Shirika la Masoko kabla soko halijaungua.

Hatua hii inakuja baada ya kukamilika kwa ukarabati na ujenzi wa ghorofa ulioanza baada ya soko kuungua July 10, 2021, ambapo na serikali ilitoa Sh29 bilioni ili lifanyiwe ukarabati ambao ulienda sanjari na ujenzi mpya wa soko dogo.

Kabla ya hatua hii, mchakato wa kutoa majina ya waliopitishwa kurejea kwenye uhakiki ulikwama July 2024 baada ya orodha ya awali kugomewa na wafanyabiashara kwa kile walichodai viongozi wao hawakushirikishwa.

Hata hivyo, ili kufikisha kilio chao hicho July 12, 2024 walikusanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kisha kuandamana hadi ofisi ndogo za Chama cha Mapinduzi, Lumumba jijini hapa.

July 13,2024 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, alikutana nao na kuridhika na hoja zao, ambapo pamoja na mambo mengine aliamuru majina 819 yaliyokuwa yamepitishwa yaondolewe kwenye mfumo na kuhakikiwa upya.

January 30, 2025 Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Hawa Ghasia, aliwaeleza waandishi wa habari kuwa uhakiki huo umeshakamilika.

TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!