MAJINA 1571 ya Walioitwa Kwenye Mafunzo Somo la Elimu ya Biashara

Filed in Kuitwa Kazini, Elimu by on May 27, 2025 1 Comment
     
MAJINA 1571 ya Walioitwa Kwenye Mafunzo Somo la Elimu ya Biashara

MAJINA 1571 ya Walioitwa Kwenye Mafunzo Somo la Elimu ya Biashara

MAJINA 1571 ya Walioitwa Kwenye Mafunzo Somo la Elimu ya Biashara

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa kushirikiana na Shirika la Educate! inatarajia kutoa mafunzo kwa walimu wa ajira mpya na kuripoti katika vituo vyao vya kazi mpaka sasa wapatao 1,571 kufundisha Somo la Elimu ya Biashara, yaani Business Studies kwa shule za sekondari za serikali Tanzania Bara.

Lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea walimu uwezo wa kutumia mbinu mbalimbali za kufundishia Somo la Elimu ya Biashara kwa wanafunzi wa kidato cha I – IV.

Mafunzo hayo yatafanyika kwa awamu tatu kuanzia tarehe 27/05-11/06/2025 katika vituo tofauti kwa muda wa siku 3 kama inavyoonekana kwenye jedwali ambatishwa hapa chini.

Pia, mafunzo yatakuwa ni “residential” ambapo walimu watalala katika kituo husika cha Mafunzo ili kuwezesha ratiba kutekelezwa kwa ufanisi.

Aidha, mafunzo yatatanguliwa na uzinduzi maalumu utakaofanyika tarehe 27 Mei, 2025 katika chuo cha Ualimu Tabora kuanzia saa 2:00 asubuhi.

Walimu waliopangwa kuhudhuria mafunzo katika kituo hiki wanapaswa kushiriki katika uzinduzi huo katika tarehe tajwa.

Walimu wote wanapaswa kwenda na vifaa vya kujifunzia kama vile kompyuta mpakato, vishikwambi, na simu janja ili utekelezaji wa mafunzo uwe na ufanisi.

Aidha, Walimu wanapaswa kubeba chandarua, taulo na shuka/blanketi kwaajili ya matumizi yake binafsi wakati wote wa mafunzo akiwa katika kituo cha Mafunzo.

Walimu watapatiwa posho maalumu ya shilingi 60,000/= kwa siku ambayo itakuwa kwaajili ya kugharamia mahitaji yao ikiwemo malazi yao binafsi katika hosteli za chuo husika.

Pia, serikali itatoa nauli na huduma ya chakula kwa walimu katika siku zote za mafunzo.

Ratiba ya mafunzo itaanza saa 2:00 asubuhi na kuhitimishwa saa 12: 00 jioni katika siku zote za mafunzo.

TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Comments (1)

Trackback URL | Comments RSS Feed

  1. Alfred swenya says:

    With thanks

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *