MAJINA ya Kidato Cha Sita Walioitwa Kujiunga na JKT Kwa Mujibu Wa Sheria 2025

Filed in Kuitwa Kazini by on May 27, 2025 2 Comments
     
MAJINA ya Kidato Cha Sita Walioitwa Kujiunga na JKT Kwa Mujibu Wa Sheria 2025

MAJINA ya Kidato Cha Sita Walioitwa Kujiunga na JKT Kwa Mujibu Wa Sheria 2025

MAJINA ya Kidato Cha Sita Walioitwa Kujiunga na JKT Kwa Mujibu Wa Sheria 2025,JKT Form Six Selection 2025, Form Six Waliochaguliwa Kujiunga JKT Kwa Mujibu wa Sheria 2025.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele, anatoa wito kwa Vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2025, kutoka Shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria Mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria kwa mwaka 2025.

Sanjari na wito huo, JKT limewapangia makambi watakayo kwenda kupatiwa Mafunzo na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 28 Mei 2025 tarehe hadi 08 Juni 2025.

Vijana hao wamepangwa katika Kambi za JKT zifuatazo; JKT Rwamkoma – Mara, JKT Msange – Tabora, JKT Ruvu na JKT Kibiti – Pwani, JKT Mpwapwa, JKT Makutupora – Dodoma, JKT Mafinga – 2 Iringa, JKT Mlale – Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba -Tanga, JKT Makuyuni na JKT Orjolo – Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila – Kigoma, JKT Itaka – Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa – Rukwa pamoja na JKT Nachingwea – Lindi.

Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (Physical Disabilities) waripoti katika Kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi Mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.

Aidha JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo.

  • Bukta ya rangi ya ‘Dark Blue’ yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, isiyo na zipu.
  • T-shirt ya rangi ya kijani.
  • Raba za michezo zenye rangi ya kijani au blue.
  • Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.
  • Soksi ndefu za rangi nyeusi.
  • Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.
  • Track suit ya rangi ya kijani au blue.
  • Nyaraka zote zinazohitajika katika Udahili wa Kujiunga na Elimu ya Juu, zikiwemo cheti vya Kuzaliwa, Vyeti vya Kuhitimu kidato cha Nne n.k
  • Nauli ya kwenda kuripoti makambini na kurudi
    nyumbani.

Orodha kamili ya majina ya vijana hao, Makambi ya JKT waliyopangiwa na maeneo Makambi hayo yalipo na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo imeambatanishwa kwenye PDF hapa chini.

Majina ya Vijana Walioteuliwa Kujiunga na Mafunzo ya JKT Kundi la Lazima (Mujibu wa Sheria) Mwaka 2025.

Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele, anawakaribisha vijana wote waliohitimu kidato cha sita mwaka 2025 kuungana na Vijana wenzao ili kujengewa Uzalendo, Umoja wa Kitaifa, kufundishwa stadi za kazi, Stadi za Maisha na Utayari wa Kulijenga na Kulitumikia Taifa lao.

TANGAZO LA KUITWA KWENYE MAFUNZO JKT 2025

TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Comments (2)

Trackback URL | Comments RSS Feed

  1. Orodha ya majina jkg

  2. ORODHA YA MAJINA JKT

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *